Usituite "wengine", sisi ni wazazi wako tuliotengana! - Harmonize amwambia Rayvanny

Rayvanny alitunga wimbo wa ghalfa jukwaani akilenga mishale kwa Harmonize na Kajala baada ya kutengana.

Muhtasari

• Mwisho wa siku, Harmonize alimsifia kwa ubunifu huo akisema kwamba Rayvanny ana talanta kubwa.

Harmonize na Rayvanny
Harmonize na Rayvanny
Image: maktaba

Bosi wa lebo ya Konde Music Worldwide Harmonize ameonekana kurekebisha uhusiano wake na Rayvanny kwa kupakia video yake akiimba kwa kumsimanga, huku akimkumbusha kuwa yeye na Kajala bado ni wazazi wake waliotengana – kwa maana ya kuwa na unyumba na Paula mtoto wa Kajala.

Rayvanny alikuwa na shoo kubwa katika mkoa wa Moshi ambapo akiwa jukwaani, alitunga tungo ya ghafla na kuiimba akilenga kumchimba mikwara Harmonize.

Kwa ustadi mkubwa, Rayvanny alitumia matukio ambayo yamekuwa yakizunguka maisha ya Harmonize na kufanya tungo, jambo ambalo japo lilikuwa linamkandia Harmonize, lakini Harmonize hakuchukulia kwa ubaya bali aliona talanta tu katika ubunifu huo.

“Kuna wengine walipakia picha kwa maringo, wakiwa gyma wananyanyua vyuma….. tena wakatoa hadi maungo ya kwenye ulingo…sasa hivi wanaweka mpaka mabango barabarani eti wako singo…” sehemu ya klipu hiyo ya Rayvanny iliimba.

Wengi walidhani Harmonize atachukizwa na hili lakini sivyo. Alikipakia klipu hicho na kumsifia Rayvanny huku akisema kwamba hapo aliona kipaji kikubwa ajabu.

“Sema wewe kaka, hivi mapenzi ni nini? Au unatakiwa ufanyeje ndio upendwe? Siwezi amini kwamba nipo singo, ila siku nyingine usituite wengine, sisi ni wazazi wako tuliotengana.  Una talanta sana Vanboy,” Harmonize aliandika kwa kumkumbusha kuwa alikuwa anatoka kimapenzi na Paula ambaye ni mtoto wa Kajala waliyetengana na Harmonize.

Wengi walidhani Harmonize na Rayvanny hawatawahi kuwa marafiki wa kupatiana shavu mitandaoni, lakini walifanya Amani baada ya kila mmoja kumfuata mwenzake Instagram, siku kadhaa baada ya kutupiana cheche za mashambulizi ya nguoni kwenye Instagram, chanzo kikiwa kutoa nyimbo zenye maudhui ya pombe.