Fahari ya mama: Mtoto wa Maureen Waititu atuzwa msanii bora wa uchoraji

Tau ni mtoto wa kwanza wa Maureen Waititu na mnyanyua vyuma Frankie Justgymit.

Muhtasari

• Waititu waliachana na Frankie miaka kadhaa iliyopita kabla ya mnyanyua vyuma huyo kuingia kwenye uhusiano na Corazon Kwamboka.

Maureen Waititu afurahi mtoto wake kushinda tuzo ya msanii bora.
Maureen Waititu afurahi mtoto wake kushinda tuzo ya msanii bora.
Image: Instagram

Mjasiriamali Maureen Waititu, ambaye ni mpenzi wa zamani wa Frankie Just GymIt ni mama wenye furaha na fahari tele moyoni.

Hii ni baada ya mtoto wake kwa jina Tau kushinda tuzo ya msanii bora wa mwaka katika kitengo cha uchoraji.

Waititu ambaye alishindwa kuzuia furaha yake alipakia rundo la picha za mtoto wake na baadhi ya kazi zake za uchoraji ambazo zilimshindia tuzo hio shuleni mwao, na kusema kuwa kupitia kwa mwanawe, alijihisi mama aliyekamilika mia fil mia.

Waititu aliwataka mashabiki wake na wanamitandao wote kutoa mapendekezo yao jinsi ataweza kuboresha hata Zaidi kipaji cha mwanawe katika uchoraji.

“Tafadhali niruhusu nishiriki wakati wa fahari wa mama 😭😭- Msanii bora wa mwaka! Ninapenda jinsi kijana huyu mdogo anavyojieleza kupitia Sanaa - hili hunifurahisha sana na ninaweza tu kuendelea kuunga mkono talanta yake. Telezesha 3/4, kidokezo tu cha kile anachopenda kuchora (Sonic) lakini hakupata nywele zangu sawa 🙈 . Ninakaribisha vidokezo vya jinsi ninavyoweza kuboresha sanaa yake,” Waititu alisema.

Waititu walitengana na Frankie miaka kadhaa iliyopita na mpenzi huyo wa kunyanyua vyuma hakukawia sana kabla ya kupata mpenzi mwingine.

Frankie aliingia kwenye uhusiano wa kimapenzi na wakili Corazon Kwamboka ambaye pia kipindi hicho alikuwa mwanamitindo wa aina yake.

Pamoja na Kwamboka, GymIt walipata watoto wawili kwa haraka kabla ya kutengana naye pia.