'Biggest Machine' Sandra Dacha atiririkwa na jasho baada ya kushiriki mazoezi gym (Video)

Dacha alionekana akijifuta jasho kwa nguo yake na kusema kwamba "sio rahisi"

Muhtasari

• Mashabiki wake walimhongera kwa kujitahidi mazoezini na kumtaka kutokana tamaa.

• Dacha alionekana kutiririkwa na kijasho akiwa ameketi kwenye kifaa cha kufanya mazoezi kwenye gym.

Mwigizaji Sandra Dacha hatimaye ametimba kwenye gym kushiriki mazoezi ya kuboresha afya na muonekano wa mwili wake.

Mwigizaji huyo anayependa kujitambulisha kama mashine kubwa kwa jina la kimajazi, alipakia video kwneye ukurasa wake wa Facebook akiwa kwenye gym kufanya mazoezi ya kunyanyua vyuma.

Katika video hiyo, Dacha ambaye ni kama tayari alikuwa ameshiriki mazoezi kwa dakika kadhaa alionekana kutiririkwa na jsho jingi mwilini, huku akihema na kulifuta jasho lile kwa kuradidi akitumia nguo yake.

Alikuwa ameketi juu ya kifaa kimoja cha kushiriki mazoezi na kuandika kwamba “Si rahisi” kuonesha ni jinsi gani watu wanaoshiriki mazoezi ya kunyanyua vyuma ili kuboresha mionekano yao hujisatiti kwa udi na ambari.

Dacha ni maarufu mitandaoni kwa kuwa mwanadada mmoja ambaye haoneshi aibu kujivunia mwili wake wa kibonge, licha ya kukejeliwa na kusimangwa na wambea wa mitandaoni.

Katika mahojiano Fulani mwaka jana, Dacha alisema kwamab alilazimika kulichukua kabisa jina la utani la “Biggest Machine” baada ya watu wengi kutumia mwonekano wa mwili wake mkubwa kumtupia maneno ya kuchukiza wakimuita mkubwa.

Aliasili jina hilo kama njia moja ya kuonesha kwamba maneno ya watu hayakuwa yanamkomoa bali ni kumjenga na kumpa ujasiri hata Zaidi wa kukumbatia muonekano wa mwili wake.

Mashabiki wake vwengi walionekana kumhimiza kutokata tamaa katika mazoezi, wakimwambia kwamba juhdi na bidi huzaa matunda mema mwisho wa kwisha.

“Ulisema lengo halikuwa kupunguza kilo za mwili bali ni kulinda afya ya mwili, lakini sasa yote mawili yanafanyika vizuri upande wako. Ni jinsi unavyoendelea, bali si kufanya vizuri kila wakati,” Mercy Nyakiti.

“Sasa uko katika njia nzuri, endelea kujitahidi Jaber,” Norah Sabai alimwambia.