Lala salama kaka-Nameless ajiunga na Wakenya kumuomboleza Kunguru

Kulingana na meneja wake wa zamani, kunguru aliaga dunia katika hospitali ya Nairobi Jumapili saa 2:00 usiku.

Muhtasari
  • Mapema leo mwanamuziki maarufu Nameless aliomboleza kifo cha Kunguru
  • Akichapisha kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii, mwanamuziki huyo alionyesha kusikitishwa na kuamka na taarifa za kusikitisha za Kunguru kupita

Tasnia ya muziki nchini Kenya iko katika majonzi kufuatia kifo cha mwanamuziki mkongwe Eric Onguru anayejulikana pia kama Kunguru.

Kulingana na meneja wake wa zamani, kunguru aliaga dunia katika hospitali ya Nairobi Jumapili saa 2:00 usiku.

Meneja huyo alifichua zaidi kwamba ugonjwa wake wa muda mrefu ulisababishwa na ajali aliyopata mwaka wa 2009 iliyoathiri uti wake wa mgongo.

Taarifa za kifo chake zimeshtua wengi na wenzake wachache wamejitokeza kuomboleza.

Akichapisha kwenye mitandao ya kijamii siku ya Philip Etale pia aliomboleza akisema kwamba wengi walifurahia muziki wake siku za zamani.

Mapema leo mwanamuziki maarufu Nameless aliomboleza kifo cha Kunguru.

Akichapisha kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii, mwanamuziki huyo alionyesha kusikitishwa na kuamka na taarifa za kusikitisha za Kunguru kupita.

Alikumbuka kuwa wote wawili walikuwa wamesajiliwa katika lebo ya muziki ya Ogopa DJs mwanzoni mwa 2000 na akafichua kuwa alikuwa ameacha kumbukumbu na vibao kadhaa.

"Oh my kuamka na kupatana na habari za kusikitisha za kifo cha Kunguru,tulikuwa tumesajiliwa wote kwenye ogopa DJs lala salama kaka umetuacha na kumbukumbuku nzuri na miziki nzuri,"Aliandika Nameless.