Sina ugomvi na Andrew Kibe, ni mwanablogu mzuri sana - Diana Marua

"Andrew Kibe ni mwanablogu mwerevu sana, ako kazini na anatafuta unga kama mtu yeyote," Marua alisema.

Muhtasari

• Kama unaeza mtaja Diana B na ujue kwamba utapata mkate, mbona usifanye hivyo? Endelea kwa sababu sisi wote tunatafuta unga,” Diana Marua.

Marua amjibu Kibe
Marua amjibu Kibe
Image: Instagram

Mwanablogu ambaye pia ni mwanamuziki Diana Marua amefunguka kwamba hana ugomvi wowote na mwanablogu mwenza Andrew Kibe hata baada ya kumtamkia laana mbaya katika wimbo wake mpya wa Narudi Soko.

Marua na Kibe kwa wiki mbili zilizopita walionesha uhasama wao mitandaoni, kila mmoja akimtupia maneno makali mwenzake, lakini Marua ameweka wazi kwamba hakuna damu mbaya baina yao bali kila mmoja ako mbioni kivyake kutafuta riziki.

“Andrew Kibe ni mkuza maudhui mwerevu sana, na unaona si rahisi kupata maudhui na unaona nani ako juu kipindi hiki, ukiona Diana B ndio ako juu sasa hivi ndio unatumia kama maudhui sioni tatizo. Kama unaeza mtaja Diana B na ujue kwamba utapata mkate, mbona usifanye hivyo? Endelea kwa sababu sisi wote tunatafuta unga,” Diana Marua alisema.

Pia aliweka wazi kwamba hakuwa anamaanisha ile laana aliyomtamkia Kibe katika wimbo wake akimwambia kwamba ‘utakufa ghetto’

Marua alisema kwamba hakuwa anamaanisha hivyo bali ni ubunifu tu wa kuweka makopa kopa kwenye wimbo wake.

Wiki mbili zilizopita baada ya Kibe kumzungumzia kwa muda mrefu akimwita kwa jina la kimajazi ‘Shosh’ Marua aliamua kujibu akisema kwa utani kwamba Kibe anapenda kumtukana bure hali ya kuwa yeye ni masikini kumliko.

Kibe alimjibu vikali akimtaja kuwa mkubwa kiumri kwa mume wake Baahti – ambao ndio ukweli Bahati aliuweka wazi kwa kusema kwamba amekubali yeye ni mtoto kwa Diana na hakuna kitu Kibe atafanya juu ya hilo kwani wao wanapendana.