Moja ya ndoto zilizotimia - Thee Pluto asema akifurahia na mtoto wake mchanga

Zoey alizaliwa mapema mwezi Novemba mwaka jana na mpaka sasa ana umri wa miezi takribani mitano.

Muhtasari

• Pluto na mpenziwe Felicity Shiru wamekuwa wakionesha hatua za makuzi ya mwanao huyo tangu kuzaliwa.

• Mpaka sasa, akaunti ya Zoey ina wafuasi zaidi ya elfu 27 kwenye mtandao wa Instagram.

Thee Pluto afurahi muda mzuri na mwanawe.
Thee Pluto afurahi muda mzuri na mwanawe.
Image: Instagram//Thee Pluto

Mwanablogu wa YouTube Thee Pluto ameonekana na bintiye mchanga akifurahia kumpakata mikononi mwake na kusema ndio moja kati ya ndoto zake nyingi ambazo zilitimia.

Pluto alionekana na bintiye Zoey karibu na ua la kijani akiwa ametokwa na tabasamu la kheri, akidokeza kwamba ni Mungu aliyemwezesha kufanikisha ndoto yake ya kuwa baba akiwa na umri mdogo.

“Moja ya ndoto zilizotimia Mungu alitimiza,” Thee Pluto alisema.

 

Mkuza maudhu huyo ambaye walitangaza kubarikiwa na mtoto wao pamoja na mpenzi wake Felicity Shiru miezi michache kuelekea mwisho wa mwaka jana, amekuwa akizua maswali mengi mitandaoni kuhusu anakotoa hela za kununua magari ya kifahari kila muda, maswali ambayo alitoa jibu lake wiki kadhaa zilizopita baada ya kupakia dhibitisho kuonesha kwamba yeye hulipwa na YouTube Zaidi ya milioni 9 kila mwaka.

Hii si mara ya kwanza Pluto anasema kuwa kuitwa baba ilikuwa ndoto yake ya muda mrefu, kwani mwaka jana baada ya kumpakata kwa mara ya kwanza, Pluto aliradidi maneno hayo akisema kwamba anajihisi tofauti na mtu aliyeboreka Zaidi.

"Nimetimiza ndoto zangu kwa kumpata mwanangu. Karibu duniani mtoto wangu @zoey_pluto Umenibadilishia jina nikawa mzazi na ukanipa heshima. Nakuombea Maisha mema. My true love ️,"Aliandika Pluto.

Katika ukurasa wake wa Instagram, Pluto alipakia picha yake na Felicity wakiwa hospitalini wakiijitayarisha kujifungua kwa mama huyo.

Zoey alizaliwa mapema mwezi  Novemba mwaka jana na mpaka sasa ana umri wa miezi takribani mitano. Mpaka sasa, akaunti ya Zoey ina wafuasi zaidi ya elfu 27 kwenye mtandao wa Instagram