Meneja wa Diamond avunja kimya Waislamu kuandika R.I.P kisa Diamond konekana kanisani

Waislamu walifurika mitandaoni kumshambulia Diamond kwa maneno makali kwa kuonekana kanisani na kunukuu maandiko ya Biblia.

Muhtasari

• Fella alimkumbusha Diamond kuhusu wimbo wa Yamoto Band kuwa 'Snitch sio mwana' akimtaka kujitahadharisha na watu wanaomsema vibaya na kisa kumchekea usoni.

Mkubwa Fella avunja kimya mashambulizi ya Waislamu dhidi ya Diamond Platnumz.
Mkubwa Fella avunja kimya mashambulizi ya Waislamu dhidi ya Diamond Platnumz.
Image: Insatgram//Mkubwa Fella

Jumapili iliyopita kulikuwa na tukio kubwa Milimani City Tanzania, tukio la mtoko wa Pasaka lililoandaliwa na wasanii wa injili Christina Shusho na Rose Muhando wakishirikiana na runinga ya Wasafi inayomilikiwa na msanii Diamond Platnumz.

Katika tukio hilo kubwa kwa Wakristo kote duniani kusherehekea kufa na kufufuka kwa Yesu Kristo, Diamond alikuwa mmoja wa wageni mashuhuri walioalikwa na kutokea kwenye ibada hiyo ya Kiksristo licha ya kuwa Muislamu.

Kutokea kwake na mpaka kunukuu baadhi ya maandishi ya Biblia kulivutia maoni mtanange kwenye mitandao ya kijamii, haswa baada ya kuonekana akiombewa na kuwekewa mikono ya Baraka na watumishi wa Mungu.

Mrengo wa dini ya Kiislamu ambapo Platnumz ni mmoja wao walijitosa mitandaoni wakiandika jumbe za rambirambi kama kwamba amefariki, kisa tu kuonekana kanisani.

Wengi wa Wailsamu mitandaoni waliandika Inna lillahi wa inna ilayhi raji'un, kauli ya Kiarab inayomaanisha ‘pumzika kwa amani’ – ishara kwamba walimuona kuwa mtu aliyeasi dini yake na malipo ya kuwa kafiri ni kifo.

Lakini sasa meneja wa msanii huyo, Mkubwa Fella amevunja kimya chake kuhusu hilo, akimhimiza Diamond kutotekwa na maneno ya watu na badala yake kuendelea kufanya kazi yake ya kutumikia dini zote pasi na ubaguzi, kwani dini zote zinaamini katika Mungu mmoja.

Fella alimshauri Diamond kuwa katika dunia, huwezi tarajia kila mtu akupende na ndio ilivyo kwamba kutakuwa na baadhi wanaokuunga mkono na wengine watatokea kukukandia mradi tu wakuone uko chini, akirejelea wimbo wa bendi ya Yamoto wanaoimba kuwa ‘Snitch sio rafiki’.

Ujumbe huu ni kwako mwanangu @diamondplatnumz duniani mpaka tukubaliane basi mwenyezi MUNGU aiweke dunia kila kitu tufanane. Na haiwezekani binadamu wanachuki mwanangu @yamotobandmusic wananyimbo Yao #snitchsiomwana,” Fella aliandika.

Katika utata unaozidi kuibuka mitandaoni, watu wamekuwa wakimkejeli Diamond kwa jinsi alivyonyolewa kwa mtindo mpya huku pia viongozi wa dini ya Kiislamu wakimtaka kuamua moja ama Ukristo au Uislam, kwa kile wanaonekana kughadhabika kuwa msanii huyo alinukuu maandiko ya Biblia katika hotuba yake wakati wa Mtoko wa Pasaka.