Davido: Mbona sikufanya collabo na msanii yeyote wa Tanzania kwenye albamu ya Timeless

Davido alisema kuwa aliogopa kushambuliwa na mashabiki wa msanii pinzani.

Muhtasari

• Msanii huyo aligusia pia jinsi mashabiki wa Nick Minaj na Lil Baby walijitosa kwenye uwanja wa mashambuliano mitandaoni baada ya kufanya collabo na Minaj.

Davido hatimaye aachia albamu yake mpya "Timeless"
Davido hatimaye aachia albamu yake mpya "Timeless"
Image: Twitter

Msanii Davido ambaye anazidi kutamba na kutambaa kwa kasi na ngoma Zaidi ya 15 kwenye albamu yake mpya ya Timeless kwa mara ya kwanza amefunguka ni kwa nini hakumshirikisha msanii yeyote kutoka Tanzania katika albamu hiyo.

Akizungumzo na Amazon Music katika podikasti ya +44 kama moja ya mahojiano anayoendelea kufanya kuisukuma hata Zaidi albamu yake, alisema kuwa anaogopa sana kufanya muziki na msanii halafu mashabiki wa msanii pinzani kwa huyo msanii waanze kumshambuli.

“Nikienda Tanzania kwa mfano na nifanye collabo na msanii huko, halafu nirudi nyumbani na nianze kuona komenti za kejeli na matusi pengine msanii huyo ana mpinzani na mashabiki wa mpinzani wake wamechizi kwamba nilikwenda huko... unajua kitu kama hicho kitakubadilisha kabisa jinsi ulivyokuwa unawaza,” Davido alsiema.

Msanii huyo aligusia pia jinsi mashabiki wa Nick Minaj na Lil Baby walijitosa kwenye uwanja wa mashambuliano mitandaoni baada ya kufanya collabo na Minaj.

Alisema kuwa Minaj alifikia hatua hata ya kumpigia simu akitaja kujua mbona mashabiki wengi walikuwa wanatimba kwenye DM yake, jambo ambalo lilifanya vigumu kufanya video ya collabo hiyo na Minaj.

Mashabiki wa Davido kwa mara nyingi hushambuliana vikali kwenye mtandao wa Twitter na wale wa Wizkid na alisema kuwa wakati mwingine hata kama hawezi kuwafikia wote, huwa anampigia simu mmoja kumtaka kuwatuliza wenzake.

Alisema kuwa kabla ya kuachia albamu yake, sehemu ya mashabiki wake walivujisha orodha ya ngoma hizo.

Mapema mwezi jana, kulikuwa na sekeseke mitandaoni kwamba msanii Alikiba alikuwa ameshirikishwa kwenye albamu ya Timeless, lakini Kiba mwenyewe alijitokeza na kukanisha waziwazi kuwepo kwenye albamu hiyo – jambo ambalo lilikuja kutokea kweli baada ya albamu yenyewe kutoka.

Mpaka sasa, Davido amemshirikisha msanii mmoja tu kutoka ukanda wa Afrika Mashariki – Diamond Platnumz ambaye walifanya remix ya wimbo wa Simba wa ‘Number One’.