Ninawaheshimu wanaume wa wenyewe-Karen Nyamu amjibu shabiki

"Waheshimu waume wa wenyewe,"Shabiki alimwambia.

Muhtasari
  • Mkenya mwenye makazi yake nchini Marekani Cosmas Ombori Ombari ambaye anafahamika sana kwa kusema ukweli bila woga wowote aliamua kumshambulia Karen Nyamu.
Image: INSTAGRAM// KAREN NYAMU

Karen Nyamu ni mwanasiasa ambaye alipata umaarufu zaidi kupitia drama zake za mapenzi akiwa na baby daddy wake Samidoh Muchoki kwani Samidoh alikuwa tayari ameoa  Eddy Nderitu.

Saa kadhaa zilizopita Karen Nyamu alichapisha kwenye ukurasa wake wa Facebook akisema anaenda kuhudhuria sherehe ambayo iliandaliwa na mzima mzima na alikuwa akiwaalika Wakenya wenzake kujumuika naye na kuhudhuria.

Mkenya mwenye makazi yake nchini Marekani Cosmas Ombori Ombari ambaye anafahamika sana kwa kusema ukweli bila woga wowote aliamua kumshambulia Karen Nyamu.

Cosmo Choy alitoa maoni yake kuhusu chapisho hilo akitumia ujumbe wa moja kwa moja na wazi ambapo alimwambia Karen Nyamu kuwaheshimu waume za watu jambo ambalo lilivuta hisia za Wakenya na vilevile Karen.

Karen alijibu hili akimwambia kwamba anawaheshimu sana na wakati huo huo anawapenda.

"Waheshimu waume wa wenyewe,"Shabiki alimwambia.

Karen alimjibu na kumwambia;

"Ninawaheshimu tena na kuwapenda."

Nyamu alikuwa miongoni mwa wanasiasa wengi walioonyesha nia ya kuwa mwakilishi wa pili wa wanawake wa kaunti ya Nairobi mwaka wa 2017 lakini alishindwa vibaya wakati wa uteuzi wa kilichokuwa chama tawala, Jubilee.

Siku ya Alhamisi, seneta huyo wa UDA alikumbuka jinsi alivyokuwa na matumaini makubwa ya kushinda kiti hicho kabla ya ndoto yake kukatizwa na kuzikwa ghafla katika hatua ya mapema ya kura ya mchujo.

"Yaani hapa nilikua najua mimi ndio next mwakilishi wa wanawake ajaye. Wapinzani wangu nilikua nawahurumia tu ni vile nilikuwa niwashinde na mbali sana😂😂😂 nikikumbuka nacheka🤣," Karen alisema.

Wakili huyo aliambatanisha ujumbe huo na picha yake ya kumbukumbu akiwa kwenye mahojiano ya televisheni.

Alikumbuka jinsi washindani wake katika kura ya mchujo ya Jubilee, Rachel Shebesh na Millicent Omanga walivyomlambisha sakafu.

"Zile Kura Shebesh alinishinda nazo!!!! Nimenyenyekea milele🙌🏽😂😂 Kati ya wagombea 11 nilishika nafasi ya 3 kwa kura 46,000. Shebesh alikuwa ameshinda kwa kura 119,000. Omanga alikuwa wa 2 kwa kura 65,000," alisema.

Mwanasiasa huyo hata hivyo alidokeza kwamba anaamini kulikuwa na mchezo mbaya ambao ulichezwa katika uteuzi huyo.