Amber Ray amwandikia mpenziwe ujumbe wa mahaba huku wakisherekea mwaka mmoja kwenye uhusiano

Alishiriki video ya chumba kilichopambwa kwa maua, na alionekana kuwa mahali ambapo likizo itakuwa.

Muhtasari
  • Wanandoa hao wanasherehekea kumbukumbu ya mwaka wao wa kwanza tangu waanze kuchumbiana.
Kennedy Rapudo na mpenzi wake Amber Ray
Kennedy Rapudo na mpenzi wake Amber Ray
Image: Instagram

Amber Ray anaonekana kutimiza ndoto yake tangu aliporudiana na mchumba wake wa sasa, Kennedy Rapudo.

Alisifu uhusiano wao kwa kuwa na kusudi na kuzingatia ukuaji.

"Tunapojitahidi kupata ukamilifu tunashindwa! Badala yake tunakua pamoja tukijiruhusu kuwa wabichi na wabaya! Kwa njia hii tayari tumekamilika! Tunahoji maisha kwa hivyo tunaishi! Hatuwahi kupigania kipande cha mkate, tunapika pai yetu wenyewe! Hatujisumbui kutafuta kusudi letu, tunazingatia kutumikia kusudi huku tukiwa wazi ili kuruhusu kusudi letu kujitokeza. Upendo ni na upendo utakuwa! Heri ya kumbukumbu ya miaka baba Africanah 🥰 na asante kwa zawadi😇."

Alishiriki video ya chumba kilichopambwa kwa maua, na alionekana kuwa mahali ambapo likizo itakuwa.

Amber Ray alifurahi sana na kumshukuru mchumba wake' kwa ishara yake ya kimapenzi. 

Anatarajia mtoto wake wa kwanza na mchumba wake', na amekuwa akimuonyesha upendo mkubwa na zawadi haswa katika kipindi hiki cha miezi mitatu ya mwisho.

Wanandoa hao wanasherehekea kumbukumbu ya mwaka wao wa kwanza tangu waanze kuchumbiana.

Wambea na mashemeji wa mitandao ya kijamii walibaki na makoko usoni baada ya mwanasosholaiti Amber Ray na aliyekuwa mpenzi wake Kennedy Rapudo kurudiana.

Amber Ray alipakia mfululizo wa picha za pamoja katika mwendelezo wa video akimtakia Rapudo kheir njema ya siku ya kuzaliwa, hivyo kufutilia mbali uvumi wa kuachana ambao waliuanzisha wenyewe.

Wiki tatu zilizopita, Amber Ray na Rapudo walitupiana maneno kwa njia za mafumbo mitandaoni huku kila mmoja akizifuta picha za mwenzake mitandaoni.