Mcheshi maarufu Butita afichua mtindo wake mpya wa nywele

Mchekeshaji huyo pia ni mwigizaji katika vipindi kadhaa za hapa nchini.

Muhtasari
  • Sadia alichapisha video zao wakicheza kwenye vilabu na hata amedokeza kuwa anatayarisha wimbo wa kumuimbia mpenzi wake.
EDDIE BUTITA
Image: INSTAGRAM

Mchekeshaji maarufu Eddy Butita amezindua staili yake mpya ya nywele. Mtumbuizaji huyo ana dreadlocks ambazo zimewasisimua mashabiki wake.

Eddy Butita anafahamika kuwa mchekeshaji maarufu nchini. Alianza katika onyesho la Churchill ambapo aliigiza kwa miaka mingi.

Alikuza jina lake baada ya kuburudisha hadhira yake kwa miaka mingi.

Butita aligonga vichwa vya habari wiki chache zilizopita. Hii ilikuwa baada ya kuingia kwenye harusi ya Akothee kwenye helikopta. Hii ilivuta hisia za wageni waliohudhuria hafla hiyo.

Mchekeshaji huyo pia ni mwigizaji katika vipindi kadhaa za hapa nchini.

Ameandika maandishi mengi ya sinema hapo awali ambayo yamefanywa kuwa sinema.

Mtumbuizaji huyo alikuwa akichumbiana na mcheshi mwenzake Mamito miaka michache iliyopita.

Walitengana na wakaamua kwenda zao. Butita sasa anadaiwa kuchumbiana na mwanamke anayeitwa Sadia ambaye aliandamana naye kwenye harusi ya Akothee.

Sadia alichapisha video kwenye akaunti yake ya Instagram akionekana kufurahia muda wake na mwanaume mwingine. Mwanamume huyo anafahamika kama Moyazy, mwanamuziki Marekani.

Sadia alichapisha video zao wakicheza kwenye vilabu na hata amedokeza kuwa anatayarisha wimbo wa kumuimbia mpenzi wake.

Mashabiki walionekana kumsikitikia Butita kwa kuachwa na Sadia.

Butita akizungumza na mtangazaji Ankali Ray alifafanua hali ya uhusiano wao.

"Hatujawahi kuchumbiana na sisi ni marafiki tu na washirika wa biashara ambao wanafanya kazi pamoja," Butita alisema.

Mcheshi huyo aliongeza kuwa wawili hao hawajawahi kukiri wazi kuwa wanachumbiana na Sadia.

"Watu walituona pamoja na wakajiamulia kwamba tunachumbiana, hakuna aliyeuliza."