"Alikiri hajui chochote!" Mwalimu wa kiingereza Diamond Platnumz avunja kimya

Diamond alitambulishwa kwa mwalimu Allan na aliyekuwa mpenzi wake Penny.

Muhtasari

• Tr Allan amemtaja mwimbaji huyo kuwa ni mwanafunzi mwenye bidii na ambaye yuko tayari kujifunza.

•Diamond pia alimuomba Allan kuwafundisha wasanii wake wengine katika WCB.

Image: HISANI

Mwalimu wa Kiingereza wa Diamond Platnumz, Tr Allan amemtaja mwimbaji huyo kuwa ni mwanafunzi mwenye bidii na ambaye yuko tayari kujifunza.

 “Mimi ni mwalimu wa Kiingereza wa Diamond Platnumz,” aliiambia Bongo 5.

Allan alisema kuwa mwimbaji huyo alimfikia alipoanza kwenda kimataifa.

"Aliniambia alitaka kufundishwa Kiingereza na hasa Kiingereza cha Marekani. Alikiri kwamba hajui chochote."

 "Nilianza kumfundisha mambo ya msingi, sasa hivi anazungumza Kiingereza kizuri sana hadharani."

Diamond pia alimuomba Allan kuwafundisha wasanii wake wengine katika WCB.

"Nilimfundisha Rayvanny, Harmonize na wengine wengi," alisema Allan.

Diamond alitambulishwa kwa mwalimu Allan na aliyekuwa mpenzi wake Penny.

"Alikutana na mimi kupitia mpenzi wake wa zamani Penny. Alipoachana na Wema Sepetu, alianza kutoka na Penny na hivyo akatuunganisha," Allan alisema

Aliongeza; "Alinilipa vizuri, ni mtu mkarimu."