Octopizzo kuwasaidia Maskini wa mtaa wa Kibra

Octopizzo kuhakikisha kuwa afadhali familia moja ama mbili katika mtaa huo wa mabanda wa Kibra utapata msaada wake.

Muhtasari

• Hali ya Uchumi imekua ikidorora kwa muda sasa, shillingi ya kenya imekua ikififia kwa dhamana dhidi ya  dolla, serikali imelazimishwa kuchelewesha mishahara ya wafanyikazi wa serikali baada ya kusongwa na madeni.

• Octopizzo pia alisema kuwa atahakikisha kuwa afadhali familia moja ama mbili katika mtaa huo wa mabanda wa Kibra utapata msaada wake.

OCTOPIZZO
OCTOPIZZO
Image: INSTAGRAM/OCTOPIZZO

Msanii Henry Ohanga almaarufu Octopizzo ameanzisha juhudi za kuwasaidia wakazi wa Kibra baada ya bei ya mfuta taa kupanda.

Hali ya Uchumi imekua ikidorora kwa muda sasa, shillingi ya kenya imekuwa ikififia kwa thamani dhidi ya  dolla, serikali imelazimishwa kuchelewesha mishahara ya wafanyikazi wa serikali baada ya kusongwa na madeni.

Msanii huyo ambaye amewai kuteuliwa kwa tuzo za Grammy alisema kuwa wakenya wengi wanaishi katika maeoneo ya mabanda na mashambani na bado wanatumia mafuta taa kupika ama mwangaza nyumbani mwao.

“Watu wanaishi katika mitaa ya mabada na mshambani wanaumia bana, na ta sai niko mtaani najaribu kuwasaidia watu wa kibra” Octopizzo alisema.

Mshindi huyo wa Tuzo za Coastal Nzumari mwaka wa 2012, alisema kuwa wakenya wengi ndio wanaoishi katika mitaa hizi na mashambani na ndio ambao wataathirika zaidi na bei ya juu ya maisha.

Octopizzo pia alisema kuwa atahakikisha kuwa afadhali familia moja ama mbili katika mtaa huo wa mabanda wa Kibra utapata msaada wake.

“Watu wanateseka na hakuna watu wanaongezewa mishahara, na juu ya hio ninahakikisha kuwa afadhali familia moja ama mbili imepata chakula kwa siku, familia moja ni kama watu 6 na nikieza wasaidia ndio furaha yangu” aliongeza Octopizzo.

Octopizzo anajitokeza baada ya bei ya mafuta taa kuongezwa na mamlaka ya udhibiti wa nishati na petroli(EPRA) baada ya ruzuku iliyowekwa na serikali ya awali kutolewa.

Bei ya mafuta taa imepanda hadi shilingi 161.13 mjini Nairobi kutoka shilingi 145.23.