Romelu Lukaku azua tetesi za kuchumbiana na rapa wa USA Megan Thee Stallion

Walionekana wakizungumza, mbali na umati wa watu, huku katika baadhi ya picha nyingine, wawili hao walionekana wakiwa wameshikana mikono.

Muhtasari

• Lautaro Martinez alifunga ndoa rasmi na mchumba wake wa muda mrefu, Augustina Gandolfo huko Como, Italia.

• Megan Thee Stallion, 28, alisemekana kuwa alikatisha uhusiano wake na mpenzi wake wa muda mrefu Pardi Fontaine mapema mwaka huu.

Lukaku aonekana katika hali ya ukakasi na Megan Thee Stallion, wazua tetesi za kuchumbiana
Lukaku aonekana katika hali ya ukakasi na Megan Thee Stallion, wazua tetesi za kuchumbiana
Image: Twitter

Mshambulizi wa Inter Milan, Romelu Lukaku ameingia kwenye vichwa vya habari tena, safari hii, kuhusu biashara yake nje ya uwanja.

Mshambuliaji huyo wa Ubelgiji mwenye umri wa miaka 29 amezua tetesi za kuchumbiana na mmoja wa wanamuziki wa kike maarufu nchini Marekani, Megan Thee Stallion.

Lukaku ambaye amezifumania nyavu mara 10 katika mechi 24 msimu huu, alionekana akiwa na rapper huyo mrembo na mwigizaji kwenye harusi ya mchezaji mwenzake wa Inter, Lautaro Martinez, na mashabiki kwenye mitandao ya kijamii wamekuwa wepesi kuhitimisha kuwa Megan Thee Stallion na mshambuliaji huyo inaweza kuwa na uhusiano wa kimapenzi

Lautaro Martinez alifunga ndoa rasmi na mchumba wake wa muda mrefu, Augustina Gandolfo huko Como, Italia.

Picha za harusi ya wapenzi hao zimeibuka kwenye mitandao ya kijamii huku mashabiki wa mshambuliaji huyo wakituma salamu za pongezi kwake na kwa mke wake mrembo mwanamitindo kwenye mitandao ya kijamii.

Harusi hiyo ilihudhuriwa na wachezaji wenzake wengi wa Lautaro huko Inter na Argentina akiwemo kiungo wa Brighton, Alex Mac-Allister ambaye anatarajiwa kuondoka Seagulls msimu huu wa joto, na Enzo Fernandez wa Chelsea.

Walakini, katikati ya sherehe za harusi, picha za mchezaji mwenzake wa Lautaro, Lukaku, na rapper maarufu wa Amerika Megan Thee Stallion pia ziliibuka kwenye mitandao ya kijamii.

Lukaku na Megan Thee Stallion ambao pia walihudhuria harusi hiyo kuu walionekana wakizungumza, mbali na umati wa watu, huku katika baadhi ya picha nyingine, wawili hao walionekana wakiwa wameshikana mikono, jambo lililowafanya mashabiki wengi kukisia kama kuna uwezekano wa kuwa na mapenzi kwenye kadi.

Megan Thee Stallion, 28, alisemekana kuwa alikatisha uhusiano wake na mpenzi wake wa muda mrefu Pardi Fontaine mapema mwaka huu.

Hata hivyo, mwimbaji huyo wa ‘Sweetest Pie’ na ‘Body’ sasa anaweza kuendelea na mchezaji wa Inter wa Ubelgiji, ingawa, si Lukaku wala Stallion aliyethibitisha kuwa wako kwenye uhusiano.

Kilicho wazi, hata hivyo, ni kwamba Megan na Lukaku ni marafiki.

Megan Thee Stallion pia hivi majuzi alihudhuria mchezo wa Serie A uliotokana na moja ya machapisho yake ya hivi majuzi kwenye ukurasa wake wa Instagram, kwani fununu zinaonyesha kuwa alialikwa na Lukaku kwenye mchezo wa Inter.