Wimbo wangu na Erick Omondi ulikuwa wa kutishia wasanii: Amber Ray

“Muziki wa Kenya haina pesa vile mimi naona kwa hivyo siwezi fanya muziki mimi,"Amber Ray aslisema.

Muhtasari

• Katika mahojiano na Plug TV Amber Ray alisema kuwa muziki haiwezi  kumumudu kimaisha kwa kuwa maisha yake yalikuwa ya bei ghali.

• Amber aliongeza kuwa muziki unamharibia wakati kwa kuwa yeye ni mtu mwenye shughuli nyingi.

Kennedy Rapudo na mpenzi wake Amber Ray
Kennedy Rapudo na mpenzi wake Amber Ray
Image: Instagram

Mwanasosholaiti Amber Ray amesema kwa majigambo kuwa hawezi kufanya muziki kwa kuwa alihisi muziki wa Kenya hauna pesa.

Katika mahojiano na Plug TV Amber Ray alisema kuwa muziki haiwezi  kumumudu kimaisha kwa kuwa maisha yake yalikuwa ya bei ghali.

Amber Ray hivi majuzi alijitokeza na kufanya wimbo aliomshirikisha Erick Omondi ambao kulingana na wawili hao iliwagharimu zaidi ya shilingi milioni 3.8.

“Muziki wa Kenya haina pesa vile mimi naona kwa hivyo siwezi fanya muziki mimi, wimbo huo na Eric ulikuwa wakuwashtua wasanii kidogo alafu nitulie.”

Amber aliongeza kuwa muziki unamharibia wakati kwa kuwa yeye ni mtu mwenye shughuli nyingi.

Mama huyo wa watoto wawili pia alijigamba na kuwa yeye hutumia Zaidi ya laki 300 kwa siku moja, hii alisema ni kabla ya kuwa katika mahusiano na mpenzi wake, Rapudo.

“Nlikuwa napitisha kiwango cha pesa nilichoweka kutumia na hio ni Zaidi ya shilingi 300,000 kwa siku moja”

Amber Ray na mpenzi wake, Rapudo walibarikiwa hivi majuzi na mtoto wa kike kwa jina Africanah Akinyi Ochieng.

Mtoto huyo mwenye miezi miwili tayari ana akaunti ya Insagram yenye wafuasi zaidi ya elfu 24 baada ya akaunti hiyo kufunguliwa wiki chache iliyopita.