Zuchu abaki na majonzi mengi Diamond akiweka wazi ushahidi wakiwa na Zari

Diamond alimshukuru Zari na wenzake kwa kufanikisha filamu hiyo ya uhalisia kuwa ya kimataifa kutokana na juhudi walizozifanya ikiwemo kiki za bifu ili kuifanya itambe.

Muhtasari

• Baddhi walimkhurumia Zuchu ambaye amekuwa akisemekana kutoka kimapenzi na msanii huyo.

• Wengine walisema kuwa hakuna vile Diamond anaweza kujitoa kwenye maisha ya Zari kwani tayari ni mama kwa watoto wao wawili.

Zari aonekana na Diamond wiki chache baada ya kumtupia maneno ya nguoni.
Zari aonekana na Diamond wiki chache baada ya kumtupia maneno ya nguoni.
Image: Instagram

Msanii Diamond Platnumz ni mtu mmoja ambaye anajua jinsi ya kuandaa kiki hadi kuwaaminisha mashabiki wake, na hivyo lengo lake la kuendelea kuzungumziwa mitandaoni kutimia.

Msanii huyo kwa mara nyingine tena amedhihirisha weledi wake katika hili baada ya kupakia picha wakiwa na mama watoto wake, Zari Hassan, wiki chache tu baada ya mjasiriamali huyo kutoka Uganda mwenye makao yake Afrika Kusini kumshambulia Diamond vikali tena kwa maneno ya nguoni kisa kubusiana na mwanasosholaiti wa Ghana, Fantana.

Diamond alipakia picha ya walioshiriki katika msimu wa pili wa filamu ya uhalisia ya Young, Famous & African kwenye jukwaa la Netflix na kuwashukuru wote kwa kuifanya filamu hiyo kuwa ya kuzungumziwa kimataifa kutokana na mbwembwe walizozua baada ya kutoka ili kuiuza.

Katika picha hiyo, Diamond alionekana amesimama kando na Zari wakiwa wametabasamiana, jambo lililowafanya wengi kuamini kwamba hata yale mashambulizi ya Zari kwake huenda yalikuwa kiki tu ili kuitambisha filamu hiyo.

“Hongera kwa watu hawa wazuri na kila mtu nyuma ya #YFA kwa kuandaa Kipindi cha Uhalisia Bora cha Ulimwenguni kwenye Netflix!…Ni Fahari sana nyinyi nyote 🌹🌍” Diamond aliandika.

Mwezi jana baada ya Netflix kuachia filamu hiyo, Diamond na Zari waliiongezea mkaa kwa kuonekana anambusu Fantana na Zari akamshambulia vikali kwa kile alisema kuwa msanii huyo alikuwa anamdanganya Fantana kuwa Zari alikuwa anamlilia kupata naye mtoto wa tatu lakini yeye akakataa.

Zari katika kile kilionekana kama kumshambulia mzazi mwenziwe, alimwambia kuwa anapotaka kutoka kimapenzi na wanawake wengine si lazima alitaje jina lake, huku akisema kuwa hakupata utajiri wake kutokana na Diamond bali alijitajirisha mwenyewe.

Baadhi ya mashabiki baada ya kuona Diamond akimpongeza Zari na wenzake, walihisi kwamba kile kilichodhaniwa kuwa ugomvi kilikuwa ni uongo na kumtuhumu kwa kutumia kiki ya bifu ili kusukuma ajenda ya YFA.

Mambo yote yalikua ni script walitupanga tuuu 😂😂😂😂 hii Ni movie akuna ureality wowote 😂😂😂😂😂 zari atabaki na diamond na wanapendana kimoyo moyo milele daima wengine wakupita tuuu” Katoto Fashion alisema.

Wengine walisema Fantana amebaki na dongo kwenye uso na wengine wakimhurumia Zuchu ambaye anasemekana kuwa mpenzi wa Diamond.