Moya David: Mbona siku hizi sifanyi surprises za kwa 'mama mbogas' sokoni

Kwenye ukurasa wake, kinyume na mwanzoni ambapo alikuwa anaonekana akiwafanyia surprise watu wa maisha ya chini, video hizo zimepungua pakubwa na alisema ni kwa nini.

Muhtasari

“Watu wengi hapa si watu wa kweli. Mtu anajifanya akona shida lakini hana. Tunatafuta watu binafsi ambao wanahitaji sana msaada" - Moya.

Moya David, ataja sababu ya kutowafanyia surprises mama mboga sokoni.
Moya David, ataja sababu ya kutowafanyia surprises mama mboga sokoni.
Image: Instagram

Alipoanza mitikasi yake, mwanatiktok Moya David alikuwa anawashtukizia watu mbali mbali wenye maisha ya chini wakiwa kwenye mishe zao na kuwachezea densi kabla ya kuwapa zawadi ya maua.

Lakini katika siku za hivi karibuni, Moya hajaonekana sana akifanya hivyo, na badala yake amekuwa akionekana katika kiwekeza Zaidi kwenye biashara zake za saluni na kinyozi kwenye mitaa ya Kilimani na Kitengela.

Katika mahojiano ya hivi karibuni na mwanablogu Eve Mungai, Moya alifunguka sababu ambazo zimempfanya kuacha kufanya kile ambacho kilimpa umaarufu – kucheza densi kwa watu wa maisha ya chini, kina mama mboga na watu wa boda boda huku wakiwa hawatarajii kabisa.

Katika ukurasa wake, kinyume na mwanzoni ambapo video nyingi tu za kupendeza akiwashtukizia kina mama mboga sokoni na kuwachezea densi, siku hizi nyingi ya video ni zile za kibiashara Zaidi.

Hata hivyo, Moya alikanusha uvumi kwamba alipata utajiri na kuwasahau watu waliomfanya kuwa maarufu kwa kuwashtukizia na maua, akisema kuwa aligundia watu wengine wenye matatizo walikuwa wanaigiza tu na kwamba siku hizi anafanya utafiti wa kutosha ili kujua mtu mwenye uhitaji wa kufanyiwa kitendo cha kushtukiziwa kwa maua na zawadi.

“Watu wengi hapa si watu wa kweli. Mtu anajifanya akona shida lakini hana. Tunatafuta watu binafsi ambao wanahitaji sana msaada. Unaona nikija nitakupa pakiti ya Unga kisha nakuacha hivyohivyo. Nikikupatia unga leo kesho utapata wapi?”

“Kwa hivyo tunatafuta wale ambao tunaweza kusaidia kwa muda mrefu. Kama ni mtu pengine hana ada ya shule, tunamsupport kupitia Moya Foundation. Kwa kweli tunafanya uchunguzi wa nyuma tunahakikisha kuwa mtu huyu anahitaji msaada,” alisema.