Jose Chameleone ashuhudiwa kwa furaha mwanawe akihitimu masomo nchini Marekani

" Hisia nzuri sana kwamba nilikuwa hapa kushuhudia hii kama nitafanya kila wakati. Hongera" - Chameleone aliandika.

Muhtasari

• “Unapoanza sura hii mpya, kumbuka daima kwamba una uwezo wa kuunda maisha yako ya baadaye na kuleta matokeo chanya kwa ulimwengu." - Chameleone alimwandikia.

Jose Chameleone ajawa na furaha mwanawe akihitimu masomo Marekani.
Jose Chameleone ajawa na furaha mwanawe akihitimu masomo Marekani.
Image: Instagram

Msanii wa muda mrefu kutoka nchini Uganda, Jose Chameleone ameonesha furaha yake baada ya mvulana wake Abba Marcus Mayanja kuhitimu kutoka shule moja nchini Marekani.

Chameleone alipakia video ya mahafali kwenye Instagram yake wakati ambapo Abba alikuwa anaitwa na kusema kuwa hakuna fahari Zaidi ambayo angeweza kujihisi Zaidi ya hiyo kushuhudia mtoto wake akihitimu.

Chameleon alifurahia na kupongeza kuhafili kwa mtoto wake kutoka Shule ya Upili ya Spring Lake Park.

“Nataka ujue jinsi tunavyojivunia wewe. Umekua kijana wa ajabu sana. Mpole, Mwenye akili na mwenye nguvu. Nataka ujue kuwa tuko hapa kukuunga mkono na kukutia moyo.”

“Kuhitimu kwako ni ushahidi wa bidii yako, kujitolea, na uvumilivu. Najua kwamba utaendelea kufaulu katika masomo yako na maishani huku pia ukiwaongoza na kuwatia moyo ndugu zako,” staa wa Valu Valu aliandika kwenye Instagram yake.

Chameleone alimtakia mwanawe mafanikio hata Zaidi katika ulimwengu  wa elimu isiyo na mwisho, akisema kuwa kama familia muda wote watakuwa nyuma ya kile atakachotaka kukisomea.

“Unapoanza sura hii mpya, kumbuka daima kwamba una uwezo wa kuunda maisha yako ya baadaye na kuleta matokeo chanya kwa ulimwengu. Jiamini, endelea kuzingatia malengo yako, na uweke moyo wako wazi kwa uzoefu na fursa mpya. Ninafurahi kuona jinsi siku zijazo zitakavyokuwa kwako, na niko hapa kukusaidia kila hatua ya njia. Hisia nzuri sana kwamba nilikuwa hapa kushuhudia hii kama nitafanya kila wakati. Hongera, Abba, na safari yako ijazwe na furaha, upendo na mafanikio,” Chameleone alimwambia.