Ni clout? Amber Ray atangaza ujio wa collabo na Drake

“Kwani tangu lini Amber akawa msanii, hiyo clout hata haijaenda shule sana, iko wazi kama meno ya ngiri,” mwingine alisema.

Muhtasari

• "Ndio nitafanya collabo na Drake hivi karibuni. Nitakuwa nachana mistari kama rapa,” Amber.

Amber Ray atangaza collabo na Drake
Amber Ray atangaza collabo na Drake
Image: Instagram

Mwanafasheni Amber Ray kwa mara nyingine amekuwa gumzo la mitandaoni baada ya kujitokeza waziwazi na kudai kwamba ahadi yake ya hapo awlai kuhusu kufanya ushirikiano wa wimbo na msanii rapa kutoka Canada, Drake bado ingalipo.

Katika video ambayo mama huyo wa watoto wawili alipakia kwenye Instastory yake akizungumza na wanablogu, alisema kuwa hajasahau ahadi hiyo yake na kusema hivi karibuni collabo yake na Drake ipo jikoni na imeiva kwa asilimia kubwa.

Alipoulizwa atakuwa anafanya nyinyi, mrembo huyo alisema kuwa kipengele chake kitakuwa ni cha kuchana mistari na kutema maneno kama rapa halisi.

“Hapo awali nilikuwa nimesema mwaka kesho nataka kufanya collabo na Drake. Ndio nitafanya collabo na Drake hivi karibuni. Nitakuwa nachana mistari kama rapa,” Amber Ray alisema.

Amber Ray anasema hili wiki moja tu baada ya yeye na mchekeshaji Eric Omondi kutangaza kwamba walikuwa mbioni kuachia collabo ya mwaka ambayo kulingana na mchekeshaji huyo, ilikuwa imegharimu kiasi cha takribani shilingi milioni nne na ilikuwa kama njia moja ya kuwaonesha wasanii wa Kenya jinsi muziki unafanywa.

Hata hivyo, ilibainika baadae kwamba ilikuwa ni kiki tu, huku baadae Ray akisema kuwa hawezi kufanya muziki nchini Kenya kwani hiyo ni njia moja ya kumanya mtu kufilisika.

Hata baada ya kutangaza ujio wa collabo yake na Drake, baadhi ya wakenya kwenye mitandao ya kijamii wamedai kwamba hiyo ni kiki nyingine ambayo Ray anajaribu kuteleza nayo ilmradi tu kubaki katika midomo ya watu mitandaoni.

“Uchumi huu umemuathiri kila mtu mpaka kimawazo...tutampa muda apone,” mmoja alisema.

“Kwani tangu lini Amber akawa msanii, hiyo clout hata haijaenda shule sana, iko wazi kama meno ya ngiri,” mwingine alisema.