Wajasiriamali Kabu Simon na Sarah Kabu sasa ni mabilionea

"Tunamshukuru Mungu kwa kuwa sasa sisi ni mabilionea. Kampuni yetu sasa ina thamani ya zaidi ya bilioni " Sarah Kabu alisema.

Muhtasari

• Simon na Sarah waliwamiminia sifa wafanyikazi wa kampuni hiyo na kusema kuwa kampuni hiyo imefika mahali ilipo kwa sasa kwa ajili ya juhudi zao.

• Wanandoa hao walifichua kuwa sasa wameingia kwenye kikundi cha mabilionea Afrika.

Sarah Kabu na Simon Kabu
Sarah Kabu na Simon Kabu
Image: HISANI

Wajasiriamali Simon Kabu na mke wake Sarah Kabu wametangaza kuwa wao ni mabilionea rasmi.

Wanandoa hao wanaomiliki kampuni ya usafiri ya Bonfire Adventures wakizungumza kwenye mahojiano na Youtuber wa Ghana Wode Maya, walifichua kuwa sasa wameingia kwenye kikundi cha mabilionea.

"Tunamshukuru Mungu kwa kuwa sasa sisi ni mabilionea. Kampuni yetu sasa ina dhamani ya zaidi ya bilioni " Sarah Kabu alisema.

Wamiliki hao wa kampuni hiyo iliyoshinda tuzo la kampuni bora nchini Kenya mwaka 2022, waliongeza kuwa walipitia wakati mgumu wakati wa Janga la Covid 19 na huo ndio ulikuwa wakati wao mgumu zaidi katika biashara yao ya usafikiri kwa miaka 15.

"Wakati wa Janga la Covid tulikuwa na wateja katika kila sehemu ya Dunia na hatungeweza kuwarudisha nyumbani kwa kuwa anga zilikuwa zimefungwa, Hasara tuliyopata kutoka wakati wa Covid ilikuwa kubwa sana. Tulienda hasara ya zaidi ya dola bilioni 2."

Kulingana na wawili hao, wanapata motisha ya kuendelea na biashara yao licha ya changamoto nyingi, kutoka kwa wafanyikazi wao na wafimilia zinazowategemea. 

Simon na Sarah waliwamiminia sifa wafanyikazi wa kampuni hiyo na kusema kuwa kampuni hiyo imefika mahali ilipo kwa sasa kwa ajili ya juhudi zao nsa biddi yao.

"Tunanyenyekea sana tunapofika ofisini na kuona watu wengi wakifanya kazi, bidii ya hawa ndio imetufikisha pahali tuko sasa. tunafanya kazi kama kikundi."

Wapenzi hao walifuchua mpango wao wa kufungua ofisi zao katika jiji la Dubai.

"Tuna ofisi 10 Kenya mzima na tunataka kufungua ofisi nchini Dubai, kwa kuwa tunapata wateja wengi wanaotaka kwenda huko"

Kampuni hiyo ya Bonfire adventures ilianzishwa miaka 15 iliyopita wakiwa wafanyikazi wawili tu, simon na mke wake Sarah na sasa wanawafanyikazi wengi .

Kampuni hiyo ya Bonfire inawafadhili wanafunzi katika shule kathaa nchini na watu wasiojiweza katika jamii.