Fahyvanny asherehekea miaka 8 ya mahusiano na Rayvanny

Wapenzi hawa walikuwa wamerudiana mwezi Aprili mwaka huu baada ya kutengana kwa muda wa miaka mitatu.

Muhtasari

• Fayvanny pia alikiri majaribu kuwepo katika mahusiano hayo, lakini akaongeza kuwa mapenzi yake kwa Rayvanny ni ya kudumu.

• Wawili hao walikumbwa na matatizo katika mahusiano haya mwaka wa 2020 na kutengana na baadaye Msanii huyo mahiri akaingia katika mahusiano na Paula Kajala.

Mwanamziki Rayvanny na mchumba wake Fahyvanny.
Mwanamziki Rayvanny na mchumba wake Fahyvanny.
Image: INSTAGRAM/ FAHYVANNY

Mwanamitindo Fayvanny au ukipenda Fayma amesherehekea miaka minane ya mapenzi yake na msanii wa Bongo Rayvanny.

Wapenzi hawa walikuwa wamerudiana mwezi Aprili mwaka huu baada ya kutengana kwa muda wa miaka mitatu.

Akionyesha mapenzi ya dhati katika video aliyopakia kwenye akaunti yake ya Instagram, Binti huyo alikiri penzi lake lisilotikisika kwa mchumba wake.

"Mimi na huyu kaka (mylife) tupogoo toka 2015 hadi sasa 2023 eeh Mungu naomba tuwe ivi ivi hadi kifo kitutenganishe,” ujumbe huo wa mapenzi ulisoma.

Fayvanny pia alikiri majaribu kuwepo katika mahusiano hayo, lakini akaongeza kuwa mapenzi yake kwa Rayvanny ni ya kudumu.

“Majaribu yanakuja na kupita, nitakupenda milele. Nakupenda.”

Wawili hao walikumbwa na matatizo katika mahusiano yao mwaka wa 2020 na kutengana,  baadaye Msanii huyo mahiri akaingia katika mahusiano na Paula mtoto wa Kajala kwa muda wa takirban miaka miwili.

Wawili hawa wamekuwa wakichimbana kwa vijembe vya nguoni kisa mwanaume, Rayvanny.

Mwanawe Kajala, Paula alizidisha mashambulizi kwa mama huyo wa mtoto mmoja baada ya kumrudia Rayvany kipindi ambacho msanii huyo aliachana na Paula.

Inaonekana ni kama Paula alishindwa kuziba pengo la Fahyma katika moyo wa Rayvanny na baada ya miaka kama miwili hivi ilimbidi msanii huyo wa Next Level Music kurudi na kumtafuta Fayma ambapo alimudhihirishia mapenzi ya kweli kwa kumshirikisha kwenye video ya ngoma yake ya Forever kama vixen wa Video.