Manzi wa Kibera adai harusi yake na mpenziwe mzee iligharimu milioni 6.8

Harusi hii inafanyika siku chache tu baada ya wawili hawa kuachana na Manzi wa Kibera

Muhtasari

• Manzi wa Kibera alisema kuwa harusi hiyo ilikuwa na wageni 12 pekee, familia na marafiki wa karibu.

• Harusi hii ilifanyika siku chache tu baada ya wawili hawa kuachana na Manzi wa Kibera kutoa sababu ya kumuachana.

Manzi wa kibera kwenye harusi yake na Nicholas Kioko.
Manzi wa kibera kwenye harusi yake na Nicholas Kioko.
Image: INSTAGRAM/ MANZI WA KIBERA

Mwanasoshalaiti Shariffa Sharon Wambui almaarufu Manzi wa Kibera amefichua kuwa iliwagharimu takriban shilingi milioni 6.8 za Kenya kufanya harusi na mpenzi wake mzee.

Katika mahojiano ya kipekee na Mpasho, Manzi wa Kibera alisema kuwa harusi hiyo ilifanyika katika kiwanja kimoja cha kuchezea Gofu katika barabara ya Kiambu.

"Harusi tulifanya katika uwanja moja wa golfu katika barabara ya Kiambu lakini sitasema ni kiwanja gani hicho, tumeamua kuiweka iwe siri kati yangu na mpenzi wangu."

Manzi wa Kibera alisema kuwa harusi hiyo ilikuwa na wageni 12 pekee na hawa walikuwa familia na marafiki wa karibu.

Harusi ambayo kufikia wakati wa kuandikwa kwa taarifa hii bado hatujapata video za harusi hiyo, iliibua gumzo mitandaoni huku mafuasi wake wakisema kuwa harusi hiyo ni kiki.

Kulingana na Manzi wa Kibera yeye na mchumba wake mwenye umri wa miaka 66 wanapanga kupata watoto wanne na wanapanga kwende Honeymoon kuanzikia wiki ijayo.

Kipusa huyo alifichua kuwa waliwasili kwenye harusi hiyo kwa ndege na alipoulizwa kwa nini hana picha yoyote wakiwasili kwenye ndege hilo alisema kwamba kurekodi au kupiga picha hakukuruhusiwa na walinzi kwenye uwanja huo.

"Tuliland na choper, lakini walinzi wa uwanja huo wa golfu hawakuruhusu kurekodi au kupiga picha tukio hilo."

Jumatano, Juni 6 Nicholas alikuwa amejitokeza na kumtaka Manzi wa Kibera kumrudishia hati miliki ya shamba lake ama warudi kwenye mahusiano na baada ya siku chache wawili hao walirudiana.

Manzi wa Kibera alisema kuwa mzee huyo anapanga kubadilisha umiliki wa shamba lile na kumpa bibi yake shamba.

Harusi hii ilifanyika siku chache tu baada ya wawili hawa kuachana na Manzi wa Kibera kutoa sababu ya kumuacha kipenzi cha roho yake kutokana na chuki na unyanyasaji aliyopokea mtandaoni.