Bahati kumpa mkewe Diana zawadi kama njia ya kuadhimisha siku ya kina baba duniani

Wakati wengi walikuwa wanadhani ni Diana ambaye angefaa kumpa Bahati zawadi ikizingatiwa kuwa ni siku ya kina baba kudhaminiwa, wanafamilia hao waliamua kufanya kinaya.

Muhtasari

• “HAPPY FATHERS DAY DIANA ❤️ Aki Nimekusubiri Unipost Nikaona Siku Itaisha! Nimeona Tuu Niku Post 🙆🙆🙆 @Diana_marua” Bahati aliandika.

Diana Marua kupewa zawadi ya siku ya kina baba na mumewe
Diana Marua kupewa zawadi ya siku ya kina baba na mumewe
Image: Instagram

Msanii Bahati Kenya ameamua kumuandikia mpenzi wake Diana Marua ujumbe wa siku ya kina baba dunaini baada ya kusubiri kwa muda mrefu bila Marua kumwandikia ujumbe huo.

Bahati alisema kuwa alisubiri Jumapili kwa muda mrefu kuona ikiwa mama wa watoto wake angepakia picha yake na kumwandikia ujumbe wa kumdhamini lakini hakuweza kuona.

Kwa maana hiyo, aliamua kumposti yeye na kumwandikia ujumbe wa kumdhamini, kama ‘baba’.

“HAPPY FATHERS DAY DIANA ️ Aki Nimekusubiri Unipost Nikaona Siku Itaisha! Nimeona Tuu Niku Post 🙆🙆🙆 @Diana_marua” Bahati aliandika.

Hata hivyo, Diana alifika kwenye chapisho hilo na kumtania mume wake kama Mamacita lakini pia kuomba radhi kwa kusahau kumpakia mume wake siku ya kina baba duniani.

“Sawa Mamaciraaa 🙆🏃️ @bahatikenya nisamehe Papito. Happy Fathers Day Mpenzi wangu ️” Diana aliandika.

Bahati alipakia picha ya Diana akiwa na watoto wao wote, na pia alisema Jumatatu alasiri atakuwa kwenye YouTube ya Marua ili kumpa zawadi.

Kulingana na Bahati, Diana alikataa kumtambua siku ya kina baba duniani katika kile alisema kuwa ni sababu hajawahi mpa zawadi yoyote tangu mwaka jana.

Diana Marua alikuwa amelalamika vikali akisema kuwa Bahati anawezaje kusema kuwa anampenda lakini hajawahi kumpa zawadi kwa Zaidi ya mwaka mmoja uliopita.

“Unasemaje kuwa unaniabudu, unanithamini, mimi ndiye kitu bora zaidi ambacho kimetokea katika maisha yako bado Zawadi ya Mwisho niliyopokea kutoka kwako ilikuwa zaidi ya Mwaka mmoja uliopita???” Diana alilalamika.