Zari amsherehekea Shakib baba wa wenyewe, ampiga chenga Diamond baba wanawe!

Zari alisema kuwa hivi karibuni anatarajia kumzalia Shakib na kumfanya kuwa baba kwa mtoto wa pili, baada ya kutambua kuwa tayari ni baba wa mtoto mmoja na mwanamke mwingine.

Muhtasari

• Zari hakuweza kumtambua Diamond hata kwa ujumbe mmoja kama baba wa watoto wake, Jumapili siku ya kina baba duniani.

• Mjasiriamali huyo alisema kuwa anatarajia kuzaa mtoto na Shakib, na kumfanya kuwa baba kwa mara ya pili.

Zari ampiga chenga Diamond siku ya kina baba, aamua kumsherehekea Shakib badala yake.
Zari ampiga chenga Diamond siku ya kina baba, aamua kumsherehekea Shakib badala yake.
Image: Instagram

Siku ya kusherehekea kina baba duniani, mwanamitindo na mfanyibiashara mkubwa, Zari Hassan alimzimia deta baba wa watoto wake wawili, Diamond Platnumz na badala yake akachagua kumsherehekea mume wake wa hivi karibuni, Shakib Lutaaya.

Zari alimsherehekea Shakib kama baba bora kwa mwanawe mmoja na mke wake wa kwanza, na kufichua kwamba anatumai hivi karibuni atamfanya kuwa baba wa mtoto wa pili.

“Heri njema ya siku ya kina baba, mpenzi wangu baba wa mtoto mmoja. Natumai nitakufanya kuwa baba wa mtoto wa pili inshaallah,” Zari aliandika kwenye picha ya pamoja na mpenzi wake.

Zari alifanya hivi kwa makusudi, na kukwepa kumtambua baba wa watoto wake wawili wadogo, Diamond Platnumz licha ya kuwa wamekuwa na wakati mzuri wakishirikiana katika malezi yao.

Mwanamitindo huyo alifunga ndoa na Shakib mwezi Aprili na mwezi mmoja baadae wakapapurana vikali na Diamond mitandaoni kwa kile alisema kuwa msanii huyo alikuwa anasema uongo katika kipindi cha Netflix, Young Famous & African.

Kwa mujibu wa Zari, Diamond alisema uongo kuwa Zari alimlilia kuzaa na yeye mtoto wa tatu, huku akisema kuwa si lazima msanii huyo alitumie jina lake katika kujinyakulia vidosho.

Zari pia alisema kuwa alikuwa bilionea wa kujitengeneza hata kabla ya kukutana na Diamond, na wala si msanii huyo aliyempa umaarufu na utajiri wake.

Hata hivyo, Zari alisema kuwa kitu pekee anachokitegemea kutoka kwa Diamond ni karo ya shule kwa ajili ya wanawe, wajibu ambao alisema msanii huyo amekuwa akitekeleza bila kufeli.