Zuchu ampa Diamond zawadi ya maua siku ya kina baba licha ya kutokuwa na mtoto naye

Diamond alijawa na hisia baada ya kugundua kwamba Zuchu ambaye hawana mtoto na yeye alimtambua kama baba ilhali Zari na Tanasha ambao wana watoto naye hawakumposti.

Muhtasari

• Msanii huyo alisema kuwa zawadi ya maua ni ya pekee kwa vile aliyempa bado hajapata kuzaa na yeye.

• Kwa upande mwingine, Zari na Tanasha ambao wana watoto wawili na mmoja mtawalia na msanii huyo hawakuweza kumuandikia ujumbe wowote.

Diamond Platnumz afichua kwa nini alishiriki kwenye video ya Zuchu.
Diamond Platnumz afichua kwa nini alishiriki kwenye video ya Zuchu.
Image: Screengrab//Zuchu

Jumapili ilikuwa siku ya kusherehekea kina baba kote duniani, na makundi mbalimbali ya watu, haswa wanawake na watoto walijitoa kwa kiasi kikubwa kuonesha mapenzi yao kwa wale ambao wanawajua kama baba kwa kuwapa zawadi ainati.

Msanii Diamond Platnumz ambaye ni baba wa watoto wanne kutoka kwa kina mama tofauti pia hakuachwa nyuma, alipokezwa zawadi, lakini zawadi yake ilikuwa tofauti kidogo kwani haikutoka kwa kwa mama wa watoto wake, bali kwa msichana ambaye hajazaa naye.

Msani Zuchu, ambaye kwa Zaidi ya miaka miwili sasa wamekuwa wakisemekana kutoka kimapenzi na Diamond ndiye alikuwa mwanamke wa pekee kumpa Diamond zawadi ya maua.

Diamond akionesha zawadi hiyo alijawa na hisia za machozi ya furaha, akisema kuwa aliishiwa na maneno ya kusema baada ya Zuchu kumpa zawadi licha ya kwamba hawajazaa na yeye.

Diamond alisema zwadi hiyo ilichagizwa kuwa yenye upekee wa aina yake, ikizingatiwa kwamba aliipokea kutoka kwa mwanamke ambaye hajapata mtoto naye, lakini alimtambua kama baba.

“Kupokea zawadi hii kutoka kwa mwanamke ambaye sijazaa na yeye ndio inaifanya kuwa hata ya upekee Zaidi. Ahsante sana Zuchu,” Diamond aliandika.

Kwa haraka, kuangalia katika kurasa za Zari ambaye ana watoto wawili na msanii huyo, lakini pia kwa Tanasha ambaye ana mtoto mmoja, hakuna kati yao aliyeweza kupakia picha ya Diamond akimtakia siku ya kheri ya kina baba duniani, kwa ajili ya watoto wao wawili.