Diamond afeki ugonjwa ili kupelekwa hospitali kukutana na madaktari warembo wa Sudan

Baada ya taarifa kuwekwa kwamba wanafunzi hao walimbwende wanaosomea udaktari kutoka Sudani wamehamishiwa Tanzania, Diamond alisema ghafla afya yake ilibadilika.

Muhtasari

• Wanafunzi hao 150 wa udaktari ni kutoka Chuo Kikuu cha Tiba, Sayansi na Teknolojia (UMST) cha Khartoum nchini Sudan.

• Walihamishiwa Tanzania baada ya machafuko ya kivita kukidhiri nchini mwao kwa zaidi ya miezi miwili sasa.

Diamond ajifanya mgonjwa kukutana na warembo wa Sudani
Diamond ajifanya mgonjwa kukutana na warembo wa Sudani
Image: Instagram

Msanii wa WCB Wasafi, Diamond Platnumz amefeki kuumwa ili kupelekwa hospitali kukutana na wanafunzi warembo kutoka Sudani ambao walihamishwa kwenda nchini Tanzania kumalizia kozi yao ya udaktri baada ya machafuko kuzuka nchini kwao Sudani.

Habari za wanafunzi hao kutoka Sudani kupelekwa Tanzania kumalizia masomo ao zilichapishwa na Millard Ayo kwenye Instagram, akisema kuwa ni maelewano kati ya mataifa hayo mawili kwamba wanafunzi hao walioathiriwa na machafuko hayo ya Zaidi ya miezi miwili, wapelekwe Tanzania kumalizia kozi zao.

Wanafunzi 150 wa udaktari kutoka Chuo Kikuu cha Tiba, Sayansi na Teknolojia (UMST) cha Khartoum nchini Sudan wamehamishiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) ili kukamilisha mwaka wao wa mwisho wa masomo,” Ayo aliripoti.

“Wanafunzi hawa wapo mwaka wa tano wa shahada ya kwanza ya utabibu, ambapo katika mwaka huo, mafunzo hufanyika kwa vitendo zaidi, hivyo Madaktari hawa Wanafujzi watafanya mzunguko (Rotation) katika idara mbalimbali ikiwemo idara ya upasuaji chini ya usimamizi wa Madaktari bingwa ili kuhakikisha wanapata maarifa yanayotakiwa” Ayo alimnukuu mkurugenzi mkuu wa hospitali ya Muhimbili.

Baada ya kupakia picha za wanafunzi hao ambao wengi walikuwa kina dada, watu mbali mbali haswa wanaume walipagawa na uzuri wao, wakisema kuwa wamependezwa sana nao na hata kujihisi kuwa wagonjwa mradi tu waruhusiwe kuingia katka hospitali ya Muhimbili kama wagonjwa ili wakutane nao.

Msanii Diamond Platnumz alikuwa miongoni mwa walioandika maoni ya kuonesha tamaa kwa njia ya utani, akisema kuwa aliamka alfajiri na kuhisi kama ni mgonjwa, huku akitaka kutibiwa katika hospitali hiyo na warembo hao.

“leo nimeamka Najiskia kama nna kahoma homa , nafkiri nahitaji vipimo Hospitali ya Taifa…” Diamond aliandika.

 Wasanii wengine pia walitangaza operesheni  ya kwenda Muhimbili kutibiwa, kama njia moja ya kuhakikisha wamekutana na warembo hao na pengine kujiombea namba na kujaribu bahati yao katika mapenzi nao kutokana na uzuri walioonekana nao.

“Naelekea Muhimbili kutoa photocopy, huwa nazipendaga stationary za pale ,” Ben Pol aliandika.