DJ Fatxo: Kwetu niliishi kujua watu wenye wametoboa masikio wanaitwa mashoga...

"Sasa venye niliona nimeishi kujihifadhi hivi vyote, halafu mnaniita kitu yenye sijawahi kuwa kwa maisha yangu, nilitoboa masikio " - Fatxo alisema.

Muhtasari

• “Niliamua kukaa maisha yangu, si kufurahisha mtu yeyote, kufurahisha tu Mungu,” Aliongeza.

• Msanii huyo alisisitiza kwamba yeye si shoga na hajawahi kujihusisha hata siku moja na ushoga, akisema kuwa yeye anachumbiana na mrembo mmoja mzuri.

DJ Fatxo afichua sababu ya kutoboa masikio licha ya dhana potovu kuhusu utoboaji wa masikio.
DJ Fatxo afichua sababu ya kutoboa masikio licha ya dhana potovu kuhusu utoboaji wa masikio.
Image: Screengrab

Kwa mara ya kwanza msanii wa Mugithi, DJ Fatxo amefichua sababu za kumfanya kutoboa masikio, licha ya watu waliotoboa masikio kuhusishwa na mambo ambayo hayajakubalika katika mila na desturi za jamii nyingi za Kiafrika.

Akuzungumza katika shoo ya KulaCooler na mcheshi Obinna, Fatxo alisema kuwa yeye amelelewa katika familia ya Wachamungu sana kiasi ya kwamba hakuwahi kujichora tattoo yoyote mwilii wala kutoboa masikio, hadi pale alipoanza kuhusishwa na kifo cha Jeff Mwathi miezi michache iliyopita.

Kulingana naye, kwao kitambo aliishi akijua kwamba watu wenye kutoboa masikio ni mashoga, na aliamua kujilinda muda huo wote ili asitoboe na kubandikiziwa kuwa shoga.

Fatxo hata alisema kuwa baada ya kifo cha Jeff amabpo pia alitajwa kuwa mshukiwa mkubwa na hata kulimbikiziwa madai mengine kuwa ni shoga na uenda kijana huyo alilawitiwa kabla ya kifo chake, aliamua kutoacha dunia imuone vile inataka na kuamua kutoboa masikio yake.

“Kwetu ukichora tattoo ni kitu kubwa sana. Kwetu ukitoboa masikio, ni kitu kubwa sana. Niliishi kujihifadhi muda huo wote ati ni juu naogopa.. Kwetu nilikuwa nasikia kitambo ati watu wenye wametoboa masikio wanaitwa mashoga. Sasa venye niliona nimeishi kujihifadhi hivi vyote, halafu mnaniita kitu yenye sijawahi kuwa kwa maisha yangu, nilitoboa masikio kusema ukweli. Nilitoboa,” Ftaxo alisema.

“Niliamua kukaa maisha yangu, si kufurahisha mtu yeyote, kufurahisha tu Mungu,” Aliongeza.

Msanii huyo alisisitiza kwamba yeye si shoga na hajawahi kujihusisha hata siku moja na ushoga, akisema kuwa yeye anachumbiana na mrembo mmoja mzuri.

“Niangalie vizuri, ninaonekana kama shoga? Mimi si shoga. Ningewataka hao wanasema hivyo wamtaje mtu mmoja ambaye nimewahi tongoza. Mimi si shoga na siwezi kuwa shoga… mimi  nina mrembo mmoja mzuri sana na tumechumbiana huu unaelekea mwaka wa pili,” Fatxo alisema.