Sylivia Saru amdai Ngesh shilingi milioni 1 kufanya collabo naye

"Anipee tu milioni moja nimfanyie tu chorus,” alisema Ssaru.

Muhtasari

Sylvia Saru amesema rapa chipukizi Mary Ngesh almaarufu Kaveve Kazoze anafaa amlipe ili aweze kushirikiana naye kimuziki..

Msanii huyo kijana alisema kuwa pia yeye hakupata mashirikiano na wasanii wenzake kwa urahisi.

Msanii wa Gengetone naye Mary Ngesh.
Msanii wa Gengetone naye Mary Ngesh.
Image: INSTAGRAM

Mwanamziki wa Gengetone Sylvia Saru amesema rapa chipukizi Mary Ngesh almaarufu Kaveve Kazoze anafaa amlipe ili aweze kushirikiana naye kimuziki.

Katika video aliyochapisha, Ssaru alisema kuwa msanii huyo ambaye amewasisimua Wakenya kwa wimbo wake 'Rieng Genje’ anahitaji zaidi ya shilingi milioni moja ili kuweza kushirikiana naye baada ya Wakenya kuwataka wasanii hao wawili kushirikiana na kufanya muziki.

"Anipee tu milioni moja nimfanyie tu chorus,” alisema Ssaru. 

Msanii huyo kijana alisema kuwa pia yeye hakupata mashirikiano na wasanii wenzake kwa urahisi.

“Ata mimi hizo collabo sikuzipata rahisi hvyo. FatherMoh unakumbuka vile ulikuwa unaninyima collabo?” Alimuuliza msaniii mwenzake aliyemshirikisha katika wimbo wake ‘Kaskie vibaya huko kwenu’.

Wimbo wake Ngesh umeweza kupata ushabiki mkubwa ata kutoka kwa viongozi wa kisiasa nchini wakiwemo Karen Nyamu na Gavana wa zamani Mike Sonko.

Seneta maalum Karen Nyamu aliisifia talanta ya Mary Ngesh Katika klipu ambayo alishiriki ambapo alikuwa akiimba wimbo ambao ulimsukuma Ngesh kujulikana. Nyamu alikuwa ameshika maneno yote ya wimbo huo.

"Ngesh anapaswa kujua kwamba Kanairo bebe anamtafuta. Hii ni aina ya talanta ambayo hatupaswi kuitazama ikipotea. Ngeshtex ni dem wa ma form na Karenzo ni wakili wa kuunda Collabo itaweza sana," aliandika Nyamu.

Licha ya kupata umaarufu kutokana na wimbo wake maarufu wa "Rieng Genje" msanii huyo alielezea changamoto anazopitia katika uimbajii ikiwa ni pamoja na ukosefu wa pesa za ada za studio na kamera ya kuunda video za kuvutia za majukwaa yake ya mtandaoni.

Gavana wa zamani wa Nairobi Mike Sonko pia alichapisha taarifa katika akaunti yake rasmi ya Twitter akiwaomba wakenya wamsaidie kumtafuta ili aweze kumpatia msaada wa kimziki.

Gavana huyo pia aliufahamau wimbo huo neno kwa neno.

“Hii ngoma imenijaz tebu nitafutieni hawa,” aliandika.