USHURU WA LAZIMA

Video: Eric Omondi aigiza jinsi wanachi wanavyolazimishwa ushuru

Mchekeshaji Eric Omondi ameeleza kwa kutumia maigizo namna serikali inavyolazimishia wananchi ushuru.

Muhtasari

•Mchekeshaji Eric Omondi ameeleza kwa kutumia maigizo namna serikali inavyolazimishia wananchi ushuru.

•Katika video, 'Mama' anaonekana kufikia kiwango cha kumfunga mchekeshaji huyo mianzi ya pua ili aweze kumeza kinywaji kile.

Image: Eric Omondi// HISANI

Mchekeshaji Eric Omondi ameeleza kwa kutumia maigizo namna serikali inavyolazimishia wananchi ushuru.

Katika kanda ya video ambayo alichapisha, Omondi ambaye alionekana kutoridhishwa na jambo hilo alijjifanya mtoto mdogo anayelazimishwa kunywa kinywaji, ambapo licha ya kulia, “mamake” alionekana kuendelea kumlazimisha kunywa na hata kumchapa.

“Kunywa! Kunywa! Nakwambia utakunywa.” Ndiyo kauli 'mama' anatoa huku Omondi akiendelea kulia.

Katika video, 'Mama' anaonekana kufikia kiwango cha kumfunga mchekeshaji huyo mianzi ya pua ili aweze kumeza kinywaji kile.

Eric Omondi aliwaachia mashabiki wake kutoa maoni kuhusu hali ya taifa kwa sasa.

Baadhi ya maoni ya mashabiki wake ni;-

@vic_banjoTusipo shikana kama wana nchi na tuweke ukabila kando hii serekeli itakuweka kwa shimo, kwa sababu kitu hawa politicians wanatuwezea ni ukabila na tukisimama na tupinge hii ujinga tutatoboa.” 

Kupitia kanda hiyo, Omondi alijaribu kueleza namna mwananchi anavyotozwa ushuru kupita kiasi, katika mswada wa fedha mwaka wa 2023 ambapo baadhi ya viongozi wa muungano tawala wamesikika hadharani wakisema kuwa utapita bila ya kubadili chochote.

Kulingana na kauli yake Rais, anasema kuwa ushuru anaoitisha Wakenya ni mdogo mno ikilinganishwa na baadhi ya mataifa yanayoendelea, ambapo siku chache zilizopita alidai kwamba, anawaitisha Wakenya 3% wabakie na 97%.

Haya yalileta utata miongoni mwa raia, kwani inafahamika wazi ushuru unaoelekezwa kutozwa iwapo mswada huo utakuwa sheria, si 3% tu bali ni zaidi na ambapo bidhaa muhimu za matumizi ya kila siku zitaendelea kupanda bei hasa kutokana na kupanda kwa mafuta ya Petroli, ambapo ushuru wake unapendelewa kuwa mara dufu ya jinsi ulivyo sasa. 

Haya janajiri wiki chache, ambapo mchekeshaji huyo aliposti kanda ya video nyingine akiwa katika barabara za London ambapo alikuwa anaomba msaada wa pesa kwa Wazungu ili kuja kuwanunulia maskini unga.