MAPENZI YA WANAMUZIKI

Bahati aeleza hisia za mapenzi kutoka kwa mpenziwe Diana

Haki Babe Punguza mapenzi utaniua! Kesho saa sita mchana naachilia wimbo wako spesheli.

Muhtasari

•Mbali na zawadi zote, alihitaji tuchukue picha kama hii kudhibitisha penzi letu ni la kweli. Wimbo spesheli nitakuwa nauachilia saa saba mchana kwako wewe mpenzi Diana.

Image: Bahati// Twitter

Tendo la  mwanamuziki Kevin Bahati lililoacha Wakenya vinywa wazi kutokana na picha alizoposti katika mitandao yake.

Katika kanda ya video na picha zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii, Bahati maarufu Mtoto wa Diana ameeleza hisia za mapenzi anazoendelea kuzihisia kutoka kwa mpenzi wake Diana.

Msanii huyo wa nyimbo za kisasa amedakia kuwa, penzi analopata kutoka kwa Diana ndilo bora zaidi huku akisema kuwa linamwuua.

“Aki Babe Punguza Mapenzi Utaniuaaa.... Diana _BahatiTomorrow 12pm I have a Special Song Dedication Dropping for You My Diana.” Aliposti katika mitandao yake ya kijamii. Ambayo katika tafsiri ni; “ Haki mpenzi wangu punguza mapenzi, utaniua. Kesho saa sita nitaachilia wimbo spesheli kwako Diana.

 Katika picha hizo, Bahati ameonekana kubebwa juu na Diana huku wakipeana busu, tukio ambalo limeibua hisia mseto miongoni mwa Wakenya.

Licha ya hayo, Bahati ameeleza kuwa zawadi haikutosha maana alimwandikia wimbo ambao alimshirikisha msanii wa Rwanda.“ A Gift was Not Enough, I Wrote for her a Song for Diana ..Drops Today at 1pm Kenyan Time featuring  KaterinaHIT Maker Bruce Melodie RWANDA KENYA COLLABO!!!” 

Bahati aliendelea kusema kuwa, hata baada ya zawadi zote hizo alizopewa, walihitaji kuchukua picha kama hiyo kudhibitisha penzi lao ni la kweli, huku akiendelea kusisitiza kuwa lazima auachie wimbo spesheli leo saa saba mchana kwa mpenziwe.

“After all the Gifts Bahati_ Diana, Still Wanted us to Take a Picture Like this to Prove Our Love is Real SPECIAL DEDICATION SONG DROPPING TODAY AT 1PM THIS ONE IS FOR YOU MY LOVE Diana.” Aliendelea kuposti.

Ambayo katika tafsiri ni kuwa, “ Baada ya zawadi zote Bahati na Diana, bado alihitaji tuchukue picha kama hii kudhibitisha penzi letu ni la kweli. Wimbo spesheli nitakuwa nauachilia saa saba mchana kwako wewe mpenzi Diana.”