Mfanyikazi wa Crazy Kennar akamatwa na polisi wakati wa kuunda makala

Kukamatwa kwa mfanyikazi huyo wa Crazy Kennar kunakuja siku chache tu baada ya mwanablogu Commentator kutiwa mbaroni kwa kurekodi filamu jijini Nairobi.

Muhtasari

•Kennar aliithibitisha tukio hilo katika picha aliyochapisha kwenye Instastory yake aliopoonekana akiwa mwenye mawazo mengi ndani ya kituo kimoja cha polisi.

Mchekeshaji Crazy Kennar akiwa kwenye kituo cha polisi.
Mchekeshaji Crazy Kennar akiwa kwenye kituo cha polisi.
Image: SCREENSHOT/CRAZY KENNAR

Mfanyikazi mmoja wa mchekeshaji Crazy Kennar amekamatwa wakati wakurekodi makala ya uchekeshaji.

Kennar aliithibitisha tukio hilo katika picha aliyochapisha kwenye Instastory yake aliopoonekana akiwa mwenye mawazo mengi ndani ya kituo kimoja cha polisi.

"Katika harakati za kuunda makala, mmoja wa watu wetu amekamatwa." Aliandika katika picha hiyo.

Mwanaume mmoja alionekana akiwa amefungwa pingu mkononi huku akiwa kororoni.

Saa chache baadaye muunda maudhui huyo alichapisha video akifurahia kuachiliwa kwa mfanyikazi wake.

Kukamatwa kwa mfanyikazi huyo wa Crazy Kennar kunakuja siku chache tu baada ya mwanablogu Commentator kutiwa mbaroni kwa kurekodi filamu katika kituo cha reli cha Railways jijini Nairobi.

Commentator alisema kuwa alikamatwa na polisi kwa sababu alikuwa ameenda kufanya mahojiano na mtu mmoja katika kituo hicho cha reli.

"Nlienda kufanya mahojiano na mtu mmoja katika kiuo cha reli cha Railways . polisi wamenishika na kuniweka ndani" aliandika Commentator.

Septemba mwaka jana, Gavana wa kaunti ya Nairobi Johnson Sakaja alitangaza kufutilia mbali leseni zote za biashara pamoja na kuondoa kwa ada zinazotozwa wapiga picha na watengenezaji filamu jijini Nairobi, kuruhusu umma kupiga picha bila malipo jijini humo.

Sakaja alieleza kuwa anatimiza ahadi yake kwa uchumi wa wabunifu kujikimu kimaisha bila kusumbuliwa na vitengo vya uslama kutokana na kutengeneza maudhui.

"Baadhi ya sheria hizi ni za kikoloni, picha inaweza kufanya nini zinapochapishwa?" Sakaja alisema.

“Tumeondoa vibali vyote vya biashara kwa wapiga picha na watengenezaji filamu wa kujitegemea jijini Nairobi. Ada zote wanazotozwa kwa siku wanapopiga picha Nairobi pia kuondolewa.”