Karen Nyamu avunja kimya kuhusu madai ya kupigwa na mpenziwe

Nyamu ambaye amewai kuwa mwathirika wa unyanyasaji wa kijinsia alisema kuwa ingekuwa ni ukweli alipigwa hangenyamaza.

Muhtasari

•Nyamu alisema maneno ambayo yanaenea mitandanoni si kweli na kuwa hatashtuliwa na watu wanaozungumza vibaya kumhusu.

•Nyamu alikanusha vikali tetesi kuwa jicho lake liliumia baada ya kuvamiwa na mpenziwe akisema kuwa hakuna mtu aliyempiga na hakuwa amaeumia jicho.

Picha zinaoenea mitandoini kuhusu Karen Nyamu kuumia macho.
Picha zinaoenea mitandoini kuhusu Karen Nyamu kuumia macho.
Image: HISANI

Seneta Karen Nyamu amekanusha uvumi unaoenea mitandaoni kwamba jicho lake lililoumia linaloonekana kwenye picha lilitokana na unyanyasaji wa kijinsia.

Akizungumza katika akaunti yake ya Facebook Jumapili, Seneta huyo wa kuteuliwa alisema maneno ambayo yanaenea mitandanoni si kweli na kuwa hatashtuliwa na watu wanaozungumza vibaya kumhusu.

"Unajua mimi si mtu wa kujali wanachosema kuhusu maisha yangu binafsi au chochote kile. Chochote unachotaka kusema juu yangu unajua unakuanga huru. Si catch sijali kwani sina issue kabisa. Kwa kweli saa zile hamniongelei nakuangaa a bit concerned."

Akizungumzia wasiwasi wa wanamitandao kuhusu jicho lake, Nyamu alifunguka kuhusu changamoto anayokabiliana nayo na kisikitika kuwa wanawake ndio wanaomvamia zaidi mitandaoni.

“So watu wanafanya jokes kuhusu gender based violence hasa watu wale hawanipendi, wanafikiri ukatili wa kijinsia ni kitu ambacho unaweza kukitumia kutatua uhasama au kitu ambacho unapaswa kuwatakia maadui zako na hawa ni wanawake. Hatuwezi kuwa wajinga hivi katika zama hizi. Unyanyasaji wa kijinsia ni suala zito, unaathiri asilimia 40 ya wanawake nchini Kenya kama vile Afrika unavyoathiri wanawake zaidi kuliko wanaume."

Mpenzi huyo wa mwanamuzuziki wa nyimbo za Mugithi, Samidoh, alikanusha vikali tetesi kuwa jicho lake liliumia baada ya kuvamiwa na mpenzi wake akisema kuwa hakuna mtu aliyempiga na hakuwa amaeumia jicho.

“Mimi binafsi nilishawahi kuwa victim huko nyuma na si mtu wa kukaa kimya kuhusu jambo kama hilo ama kuficha na kama kuna mtu mmoja mkweli baada ya Riggy G katika nchi hii ni Karen Nyamu.Hivyo si kitu naeza nyamazia."

Mwanasiasa huyo anayezingiriwa na utata mitandaoni alisema kuwa alizungumza na mtu ambaye kulingana naye ndiye angeweza kumuumiza kama ingekuwa kweli alikuwa ameumia macho na mwanaume huyo akafutilia mbali madai hayo.

"I have raised it with the person who could have been the person who people think has hit me, ameniambia ah we lenga uciu ni wana (In kikuyu to mean its nonsense) you know how we dismiss things every other thing that is said about us."