Kuna muda Stevo akashindwa kufanya muziki kwa kuzozana na mkewe - uongozi

“Sisi hatukuenda ndani sana kujua nini kiliendelea na mke wake, tulichokiangalia Zaidi ni afya yake, afya yake ya kiakili, tulihakikisha kila muda alikuwa studioni, alikuwa na uhuru" - MIB.

Muhtasari

• Kiongozi huyo aidha alisema kuwa Stevo hakuwahi kuelezea sana kilichokuwa kinaisibu ndoa yake.

• “Siwezi zungumza mengi kumhusu mwanamke wake kwa sababu siko karibu sana naye na huwa hatuna mazungumzo sana" - MIB.

Uongozi wa Stevo Simple Boy umefichua madhira ya ndoa ambayo yalimkuta Stevo baada ya kumuoa Grace.
Uongozi wa Stevo Simple Boy umefichua madhira ya ndoa ambayo yalimkuta Stevo baada ya kumuoa Grace.
Image: Instagram

Uongozi wa msanii Stevo Simple Boy umefichua kwamba msanii huyo aliwah kumbwa na tatizo la msongo wa mawazo baada ya kuzozana vikali na mwanamke ambaye anamtaja kuwa mkewe, Grace Atieno.

 Katika mahojiano ya kipekee kwa njia ya Simu na Radio Jambo, mmoja wa viongozi wa Men In Business – MIB – ambao walikuwa wanasimamia kazi za msanii huyo alifunguka kuwa msanii huyo aifika kipindi akashindwa hata kufanya kazi za muziki katika kile walisema kuwa alipatwa na msongo wa mawazo.

Kwa mujibu wa kiongozi huyo wa MIB, Stevo alikuwa amezozana na kuvurugana na mkewe kiasi kwamba aliathirika kimawazo.

“Siwezi zungumza mengi kumhusu mwanamke wake kwa sababu siko karibu sana naye na huwa hatuna mazungumzo sana. Mimi nakumbuka mara ya mwisho Stevo alikuwa katika kipindi kigumu cha msomgo wa mawazo, watu hawakujua. Walikuwa na tofauti zao na mwanamke huyo anayemuita mke wake, nakumbuka hata wakati huo Stevo alishindwa kuingia studioni na tulikuwa tunafanya kazi sana kumzungumzia,” kiongozi huyo alisema.

Kiongozi huyo aidha alisema kuwa Stevo hakuwahi kuelezea sana kilichokuwa kinaisibu ndoa yake lakini pia wenyewe hawakuwa wanaunga mkono wazo lake la kuwa na mke kwani walikuwa wanamtaka kwanza kujibidiisha kisanaa kabla ya kutafuta mrembo.

“Nilimuuliza na aliniambia kwamab wanazozania mambo ya hapa na pale, sikuelewa sana kwa sababu mimi nilikuwa natilia mkazo Zaidi upande wake wa kibiashara na nilimwambia Stevo ni lazima uzingatie kazi zako kiasi kwa sababu kazi ambazo ziko mbele yetu, tunahitaji kuwekeza bidii Zaidi ili kuwahi dili nono lenye linaweza likabadilisha maisha yako,” alisema.

“Sisi hatukuenda ndani sana kujua nini kiliendelea na mke wake, tulichokiangalia Zaidi ni afya yake, afya yake ya kiakili, tulihakikisha kila muda alikuwa studioni, alikuwa na uhuru wa kuja kwangu muda wowote na kuzungumza chochote kilichokuwa kinamsibu,” aliongeza.

Alisema kuwa amemfanyia msanii huyo makubwa, mengine ambayo hata hayakuwa ndani ya mkataba wao wakati walimchukua mwaka mmoja uliopita.