INJILI ZA EMBARAMBAMBA

Niliweka mahubiri ya pasta Ezekiel YouTube yangu, kikaniramba - Embarambamba

Niliona mahubiri yaliyonigusa akiwa gerezani, nikayaweka kwa Channel yangu kikaniramba - Embarambamba

Muhtasari

• Mwimbaji huyo akizungumza katika mahojiano ya simu na Radio Jambo, alieleza kuwa akaunti hiyo ilikuwa imefutwa na Mhubiri Pastor Ezekiel, ila siku ikarejeshwa Juni 25 aliposihi arejeshewe.

Image: INSTAGRAM// EMBARAMBAMBA

Mwanamuziki wa nyimbo za injili kutoka Kisii,  Christopher Musyoma maarufu  Embarambamba amefunguka sababu zilizochangia kufutwa kwa akaunti yake ya Youtube.

Mwimbaji huyo akizungumza katika mahojiano ya simu na Radio Jambo, alieleza kuwa akaunti hiyo ilikuwa imefutwa na Mhubiri Pastor Ezekiel, ila siku ikarejeshwa Juni 25 aliposihi arejeshewe.

“Ilirejeshwa jana, nilienda kuweka mahubiri ya Ezekiel, saa ile alitoka gerezani kuna mahubiri yake yalinigusa sana, akasema vile Mungu anaweza kuinua mtu kutoka Zero mpaka unaheshimiwa, sasa hiyo mahubiri nikaenda kutoa kutoka chanel yake nikaweka yangu, plus kuna ingine nilikuwa naongea juu yake vile Mungu amekusaidia. Hiyo ndiyo ilinipea strike hadi channel yangu ikaenda.”  Alisimulia Embarambamba.

Kulingana na kauli yake, alikiri kuwa Mhubiri Ezekiel hataki kazi yake isambae na ienee kwa wengine, “Hataki mtu anashare kitu chake.” Aliendelea.

Mwanaume huyo wa watoto watano aliendelea kueleza kuwa, Ezekiel aliona sketi akaongea naye na kumweleza kuwa Wakisii ndio walimtetea mahakamani, na ni wao walifanya kesi yake ikawa nyororo alipokiri kuwa ni majirani na hajakosana.

“Ni hiyo tu, akaona hiyo kitu nimeweka skirt, niliongea tu nikamwambia sisi Wakisii ndio tulikusupport kwa Court, sisi ndio tulifanya kesi yako ikawa nyororo , hatujakosana na tena sisi ni majirani kutoka Kisii na unahitaji unirudishie channel yangu kwa sababu mimi sijavunja laini yako.”  Alisema.

Mwimbaji huyo  mwenye utata alionekana akidensi na kucheza miondoko ya kustaajabisha huku akiwa amevalia sketi fupi ya kahawia na blauzi nyekundu, katika video zake za hivi karibuni.

Tukio la kudensi kwa kutumia mavazi ya wanawake liliibua hisia mseto, kwani wanamitandao wengi walihisi mwanamuziki huyo mwenye umri wa miaka 35 alienda kinyume na matarajio ya wengi hasa ikifahamika kuwa anajitamburisha kama msanii wa nyimbo za injili.