Nimetoka Tandale na kuaminiwa, ukiwa mtumizi wa dawa za kulevya huwezi aminiwa - Diamond

"Ukiwa unatumia dawa za kulevya unaitwa teja hakuna ambaye atakupa kazi, hakuna ambaye atakupokea hata katika muziki" - Diamond.

Muhtasari

• Ujumbe huo wa Diamond ambaye pia ni Mkurugenzi wa Wasafi Media, ulishangiliwa na mamia ya watu ambao wanashiriki katika maadhimisho hayo.

Diamond aingia vitani dhidi ya dawa za kulevya.
Diamond aingia vitani dhidi ya dawa za kulevya.
Image: Facebook

Nyota wa muziki wa kizazi kipya Afrika, Nasibu Abdul maarufu Diamond Platnumz ameingia kwenye vita ya kupambano dhidi ya matumizi ya dawa za kulevya kwa kuwataka vijana kuachana matumizi ya dawa za kulevya kwani hazina manufaa yoyote katika maisha yao.

Diamond alizungumza hayo wikendi iliyopita katika maadhimisho ya kitaifa ya kupinga matumizi ya dawa za kulevya katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jumapili mbele ya Rais Samia Suluhu Hassan huko Arusha.

Kwa mujibu wa msanii huyo, dawa za kulevya licha ya kuharibu afya pia uvutaji unaondoka fursa kwa vijana.

"Ukiwa unatumia dawa za kulevya unaitwa teja hakuna ambaye atakupa kazi, hakuna ambaye atakupokea hata katika muziki sisi tukikuona tunakuona teja tu," mkurugenzi mtendaji wa WCB Wasafi alisema.

Alisema hakuna faida yoyote katika dawa za kulevya na matumizi yake yanaondoa ndoto za kuishi vizuri wala kuaminiwa katika jamii ikiwepo kupata kazi.

Msanii huyo alijitumia kama mfano akisema kuwa kijana ukijituma na kukwepa dawa za kulevya utaaminiwa na kupewa fursa za kuzungumza mbele ya watu wenye heshima, akisema kuwa yeye angekuwa mtumizi wa dawa za kulevya hakuna ambaye angemjua Zaidi ya marafiki zake katika mtaa wa mabanda wa Tandale alikokulia.

"Leo mimi nimetoka Tandale nimefika Arusha kwa sababu naaminiwa," amesema Diamond.

Ujumbe huo wa Diamond ambaye pia ni Mkurugenzi wa Wasafi Media, ulishangiliwa na mamia ya watu ambao wanashiriki katika maadhimisho hayo.

Ikumbukwe wiki chache zilizopita, rais Hassan pia alimteua Diamond miongoni mwa wasani wengine katika baraza ya vita dhidi ya Malaria nchini Humo.