Pigo kwa Stevo Simple Boy menejimenti yake ikivunja mkataba wake

Uongozi huo uliendelea kumtaka mwimbaji huyo kushirikiana nao katika kipindi hiki cha mpito ili kufanikisha mchakato mzima.

Muhtasari

• Katika barua kwa mwanamuziki Stephen Otieno Adera almaarufu Stevo Simple Boy, wasimamizi hao walisema kuwa wamekatisha mkataba wao wa kimuziki na msanii huyo.

Stevo simple boy.
Stevo simple boy.
Image: Instagram

Wasimamizi wa mwanamuziki kutoka Kibera, Men In Business (MIB) waemtangaza kusitisha kwa mkataba baina yao na mwanamuziki Stevo Simple Boy.

Katika barua kwa mwanamuziki Stephen Otieno Adera almaarufu Stevo Simple Boy, wasimamizi hao walisema kuwa wamekatisha mkataba wao wa kimuziki na msanii huyo.

"Tunapenda kukuarifu kuwa hatutaki tena kuendelea na mkataba wetu wa muziki na wewe. Barua hii ni taarifa kukuelezea nia yetu ya kusitisha mkataba huo kwa njia halali na kwa mujibu wa itifaki ya kisheria," ilisome sehemu ya barua hiyo.

Uongozi huo uliendelea kumtaka mwimbaji huyo kushirikiana nao katika kipindi hiki cha mpito ili kufanikisha mchakato mzima.

"Kusitishwa kwa mkataba kutaanza tarehe 31 Julai hivyo tuna siku 35 za kuwasilisha maslahi ya pande zote mbili kwa ajili ya mabadiliko ya haraka."

Jumamosi, mke wa mwimbaji huyo, Grace alimwambia mwanablogu Vincent Mboya kwamba walikuwa wameteseka kwa muda sasa na ata wawili hao walilazimika kulala bila kutia chochote kinywani.

“Watu wengi wanadhani Stevo ndiye anaendesha kurasa zake za Tiktok na Instagram lakini nataka mfahamu kuwa si yeye, wengi wanalalamika kutaka kumsaidia lakini hapatikani."

Grace alifichua kuwa licha ya swala hili kuwa gumu kwake kuzungumzia hatharani ilimlazimu kujitokeza na kuomba msaada kwa kuwa walikuwa wakiteseka. 

"Inaniuma kuongelea hili. Hana chochote. Watu wanadhani anaishi maisha mazuri lakini anajitahidi. Anajitahidi, unaweza kuwasiliana naye au kumtumia msaada wowote wa kifedha. Atathamini sana.Yani anaumia sana. Mi nikijaribu kuongea like ..pain injini kali sana. Sijui mtamsaidia vipi hana chochote." alisihi Grace.