Zari afichua sababu ya kususia White Party ya Birmingham, UK licha ya kufika mapema

"Nilikuwa nimeketi kwenye chumba change cha hoteli nikisubiri baada ya ahadi nyingi, haikutokea,” Zari aliandika

Muhtasari

• Zari alionekana akiwa anajivinjari kwa picha na mumewe Shakib Cham na kusema kuwa hakuna vile angejishusha na kujitokeza licha ya promota kugomba kufikia matakwa yake.

Zari ataja sababu za kususia White Party.
Zari ataja sababu za kususia White Party.
Image: Facebook

Mwanasosholaiti Zari Hassan amefichua sababu zilizomfanya kususia kutokea katika shoo ya Birmingham huko Uingereza ambapo alikuwa anatarajiwa kutokea wikendi iliyopita.

 Zari ambaye amekuwa akiipiga debe shoo hiyo alitarajiwa kuonekana Wikendi iliyopita na alisafiri hadi nchini Uingereza lakini hakuweza kutokea kama ilivyopangwa na sasa ametoa maelezo kwa mashabiki wake ambao aliwafeli kwa kutotokea.

Kwa mujibu wa mjasiriamalai huyo mkubwa mwenye makaazi yake nchini Afrika Kusini, alisalia tu kwenye chumba chake cha hotelini baada ya promota wa shoo hiyo kukosa kuafikiana na matakwa yake.

“Radhi zangu kwa kila mtu ambaye alitokea jana kwenye White Party ya Birmingham kuniona lakini hawakuweza kuniona. Kwa bahati mbaya, promota hakuweza kuafikia na matakwa yangu ya kimkataba na nimehisi kutamauka kama kila mtu kwa sababu nilikuwa nimeketi kwenye chumba change cha hoteli nikisubiri baada ya ahadi nyingi, haikutokea,” Zari aliandika kwenye Instastory yake.

Zari alionekana akiwa anajivinjari kwa picha na mumewe Shakib Cham na kusema kuwa hakuna vile angejishusha na kujitokeza licha ya promota kugomba kufikia matakwa yake.

Hata hivyo, aliwaahidi mashabiki wake kuwa wakati mwingine wataweza kumuona wakati promota ataweza kupanga na kuafikia na kila kipengele katika mkataba wake.

Ikumbukwe Zari ni mmoja kati ya wanawake maarufu barani Afrika na alijumuishwa kweney kipindi cha uhalisia cha Young, Famous & African kupitia mtandao wa Netflix ambacho kilikuwa kinawajumuisha vijana wenye utajiri mkubwa lakini pia na umaarufu.