Gaucho afichua sababu kuu ya kuchukia kuvaa suti hata wakati atachaguliwa

"Sio vibaya kuvaa suti, lakini hakuna kitu kibaya kama mtu amevaa suti akiomba nauli.” - Gaucho alisema.

Muhtasari

• Aliwasuta baadhi ya watu ndani ya muungano wa Azimio wanaompiga vita kwa vile yeye huvalia mavazi ya kawaida na kuwa hana gari la kifahari kama wao.

 

Gaucho akana mapenzi kwa suti
Gaucho akana mapenzi kwa suti
Image: Facebook

Mtetezi mkali wa sera za Azimio na kinara wao Raila Odinga, Calvince Gaucho amefichua kwa nini hawezi kuvalia suti hata apate cheo cha juu kiasi gani.

Kulingana naye, amezoea kuvalia mavazi ya kawaida ambayo yanamweka kwenye ngazi sawa na vijana anaowaongoza kama rais katika vuguvugu la bunge la wananchi, na kuvalia suti kutakuwa kunamtenga mbali na vijana wengi ambao wanachukulia mtu mwenye suti kama mwenye utajiri wa juu.

Gaucho pia alitaja sababu nyingine ambayo inamfanya kutoendekeza mapenzi yake kwa suti kuwa, ni bora avae mavazi ya kawaida na anasaidia watu kuliko kuvaa suti na kuwajengea watu picha vichwani kuwa ana hela ilhali uhalisia wa maneno naye ni ombaomba wa nauli kumfikisha nyumbani mwisho wa siku.

“Suti mimi sitaki kuvaa kwa sababu mavazi kama haya ya kawaida ndio hunifanya nakuwa karibu na wale vijana ambao mimi nawaongoza. Sio vibaya kuvaa suti, lakini hakuna kitu kibaya kama mtu amevaa suti akiomba nauli.”

 Afadhali kama mimi hivi sasa nikikuomba mia utaona enyewe suruali yangu imeraruka inaniruhusu kuomba nauli. Lakini mimi nikija na suti pamoja na tia, utaniamini kweli?” Gaucho alitania.

Aliwasuta baadhi ya watu ndani ya muungano wa Azimio wanaompiga vita kwa vile yeye huvalia mavazi ya kawaida na kuwa hana gari la kifahari kama wao.

“Mimi niko Azimio, ni vile tu mimi wananidharau kwa sababu hizi suruali navaa zimeraruka. Hawaamini mtu hana V8, mtu havai suti,” Gaucho alisema.