Harmonize aliniambia anataka nifanye collabo naye, akanihepa - Embarambamba

Alinipigia simu akaniambia ako na shughuli nyingi wacha arudi Tanzania tutaongea

Muhtasari

• Lakini hawa wasanii wadogowadogo makabila nimefanya collabo na wao wengi.

•  Nimefanya na msanii mmoja kutoka Kalenjin kwa President,saa hii wimbo tulifanya iko 2 million

Image: Embarambamba//Facebook

Msanii wa nyimbo za injili Chris Embarambamba ameeleza kuwa alikuwa na nia ya kushirikisha mwanamuziki wa Bongofleva Harmonize, katika muziki wake.

Katika mahojiano na Radio Jambo Juni 26, mwimbaji huyo alikiri kuwa nchini Kenya kwa wasanii mashuhuri hajapata kuwashirikisha katika muziki wake ila Harmonize, walizungumza kuhusu biashara hiyo.

“Kutoka Kenya wale wasanii wakubwa hatujafanya collabo na wao , lakini ni ile Harmonize alikuja Kenya akasema anataka kufanya collabo na mimi halafu akanipigia simu akaniambia ako na kazi nyingi wacha arudi Tanzania ata organize.” Alisimulia mwimbaji huyo.

Aliendelea na kukiri kwamba, wasanii wadogowadogo nchini tayari amekwisha kuwashirikisha katika muziki wake.

Lakini hawa wasanii wadogowadogo makabila nimefanya collabo na wao wengi. Nimefanya na msanii mmoja kutoka Kalenjin kwa President,saa hii wimbo tulifanya iko 2 million, kuna mwingine Kalenjin hapo wa Gospel, huyo ni mwanamuziki tulifanya, kuna mwingine wa Gospel, wimbo yake iko 1 million point na huyu wa huko  Nandi Eldoret hii tulitoa ya juzi inasema ‘Nataka Nikuingize Ndani‘ pia hiyo ilisonga sana.

Mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 35 alidakia kuwa nyimbo anazoimba ni njimbo za injili ila ndani yake anajaza ucheshi, ambapo alitoa mifano ya nyimbo zake zenye ucheshi ndani yake.“ Kwa mfano katika huu wimbo wa Nataka Nikuingize Ndani mtu akiusikiza atafikiria mambo ingine, ila namaanisha nataka nikuingine ndani ya Yesu.” Aliendeleza.