Kesi ya Michael Jackson kumlawiti dancer wake yafufuliwa miaka 13 baada ya kifo chake

Katika kesi ya Robson, dancer huyo alidai kuwa MJ alimnyanyasa kingono kuanzia umri wa miaka 7 hadi alipokuwa na umri wa miaka 12

Muhtasari

• "Alinifanya nijisikie kuwa mshiriki, kwamba nilitamani angalau kama sio zaidi yake." - Robson aliambia jarida la Guardian.

Kesi ya MJ dhidi ya ulawiti yafufuliwa tena.
Kesi ya MJ dhidi ya ulawiti yafufuliwa tena.
Image: BBC NEWS

Michael Jackson aliaga dunia tarehe 25 Juni, 2009 na imepita miaka 13 tangu kifo chake lakini bado baadhi ya mambo aliyotuhumiwa kutekeleza kwa watu waliokuwa wanamzunguka yanazidi kumwandama hadi kaburini, Zaidi ya muongo mmoja baadae.

Inaarifiwa kwamba aliyekuwa mcheza densi wake kwa jina Wade Robson ameelekea mahakamani kwa mara nyingine tena akitaka kufufuliwa kwa kesi ambapo anamtuhumu msanii huyo nguli wa muziki aina ya Soul na Pop kumlawiti mara kadhaa kipindi cha uhai wake.

Kwa kuwa Michael Jackson aliaga dunia kabla ya kesi yoyote ya mahakama, Robson alishtaki kampuni ya nyota huyo wa pop mwaka wa 2013, kisha kesi hiyo ikatupiliwa mbali mwaka wa 2017 baada ya hakimu kuamua kuwa iliwasilishwa kinyume na sheria ya vikwazo.

Licha ya kesi hiyo kutupiliwa na kampuni ya Jackson kushinda, Robson alionekana kutotulia na mwaka huu 2023, sheria mpya inayoongeza muda kwa watoto walioathiriwa kuwasilisha madai yoyote ya kisheria inamrejeshea Robson fursa ya kwenda mahakamani.

Kwa mujibu wa jarida la WallStreet, Kesi hiyo ilipotupiliwa mbali, kampuni ya Michael Jackson ilisema kuwa "Wade Robson ametumia miaka minane iliyopita kutafuta madai ya kipuuzi katika kesi tofauti dhidi ya kampuni ya Michael Jackson na makampuni yanayohusiana nayo. Robson amechukua karibu dazani tatu na kukagua na kuwasilisha maelfu ya nyaraka zinazojaribu kuthibitisha madai yake, lakini Jaji kwa mara nyingine tena ameamua kwamba madai ya Robson hayana uhalali wowote, kwamba hakuna kesi inayohitajika, na kwamba kesi yake ya hivi punde imetupiliwa mbali."

Katika kesi ya Robson, dancer huyo alidai kuwa MJ alimnyanyasa kingono kuanzia umri wa miaka 7 hadi alipokuwa na umri wa miaka 12, akidai kuwa "Michael Jackson alikuwa mmoja wa watu wema na wapenzi niliowafahamu. Alinisaidia sana katika kazi yangu na yangu. ubunifu. Pia alininyanyasa kingono kwa miaka saba."

Robson pia alizungumza na jarida la The Guardian na kudai kwamba "Alinifanya nijisikie kuwa mshiriki, kwamba nilitamani angalau kama sio zaidi yake. Na jambo ni kwamba, unyanyasaji haukujisikia ajabu kwa sababu ulikuwa ukifanywa na mtu huyu aliyekuwa kama mungu kwangu. Mengi yake yalikuwa uthibitisho kwangu. Lakini hiyo inamaanisha nini, kwamba niliipenda? Kama, mimi ni kituko pia."

Kampuni ya Michael Jackson imekanusha kabisa madai na makosa yote yanayodaiwa na washtaki.