Mike Sonko anogesha mtindo wake wa mavazi kusherehekea Eid-al-Adha

Muhtasari

• Katika mtandao wa Instagram na TikTok, mwanasiasa huyo mkwasi alipakia video akiwa amesimama tisti kwenye vazi hilo huku akikariri punje za tasbihi kwa swala.

Mike Sonko apiga luku safi kusherehekea Eid-Al-Adha.
Mike Sonko apiga luku safi kusherehekea Eid-Al-Adha.
Image: Twitter

Gavana wa zamani wa Nairobi Mike Sonko amewaacha Watumizi wa mitandao ya kijamii kwa nyuso zenye furaha baada ya kuonesha ubunifu wake kwa mara nyingine katika fasheni yake ya mavazi.

Mfanyibiashara huyo safari hii alitokea na vazi a Kiislamu maarufu kwa jina Kanzu ambalo liliwafurahisha wakenya kwani lilikumwa limepambwa kwa rangi za bendera ya Kenya.

Wengi walimtaja Sonko kama mzalendo kwa kuvalia vazi lenye nembo ya bendera ya taifa, huku akijumuika na jamii ya Waislamu humu nchini kusherehekea siku kuu ya Eid-al-Adha.

“Upekee wa Eid hii ulete furaha nyingi, upendo na furaha maishani mwenu. Mwenyezi Mungu awabariki kwa furaha yote mnayostahili. Eid ul adha Mubarak! Mwenyezi Mungu azikubali dua zenu zote na awapeni maghfira katika Eid hii,” Sonko aliandika kwenye Twitter.

Siku ya Eid-al-Adha ikiwa ni ya kipekee kwa Waislamu kusherehekea Ibrahim kutoa dhabihu ya mwanawe Isaq kwa Mungu kabla ya Mungu kumshusha kondoo badala yake, Sonko pia alishiriki video ya watu wenye majoho meupe ya Kiislamu wakiwa wameshika mbuzi wakiwavuta kuelekea kuchinjwa.

Katika mtandao wa Instagram na TikTok, mwanasiasa huyo mkwasi alipakia video akiwa amesimama tisti kwenye vazi hilo huku akikariri punje za tasbihi kwa swala.

Bilas haka Sonko kutokea na muonekano wa kipekee si jambo geni, mwanasiasa huyo anafahamika sana kwa weledi wake na upekee katika fasheni yake ya mavazi, ikiwemo mikufu yake ghali shingoni na pete za dhahabu kwenye vidole vyote vya mikono yake.