"Mwamba huyu hapa!" Karen Nyamu amkumbatia Samidoh mbele ya familia yake

“Hata kama ni wewe familia ya Samidoh utachagua pesa ama 'Nothing but prayers'?” mwanamitandao mmoja aliandika akionekana kurejelea kwenye kauli ya Edday na ukwasi wa Nyamu.

Muhtasari

• Wanafamilia wa Samidoh pia walionekana kufurahia uwepo wa Nyamu miongoni mwao.

• Picha hizo ziliwaacha mashabiki katika mgawanyiko wa maoni, makundi mawili yakionekana kuibuka - lile la kusimama na Edday na lingine la kumtetea Nyamu.

Karen Nyamu amkumbatia Samidoh mbele ya wanafamilia wake.
Karen Nyamu amkumbatia Samidoh mbele ya wanafamilia wake.
Image: Instagram

Karen Nyamu anazidi kujinafasi katikati mwa familia ya mwanamuziki Samidoh, huku akitumia nafasi hiyo vizuri katika kipindi hiki ambacho mke wa kwanza wa Samidoh, Edday Nderitu yuko nchini Marekani kwa miezi kadhaa sasa.

Nyamu alipakia rundo la picha kwenye Instagram yake akionesha jinsi walivyojumuika pamoja na wanafamilia wa mpenzi wake Samidoh kumsherehekea kijana mmoja aliyekuwa amevalia joho la kufuzu chuo kikuu – kuashiria kwamba sherehe ilikuwa kumsherekea kijana huyo.

“Jana usiku tulikusanyika kusherehekea kijana mmoja wa kufurahisha na mzuri. Hongera kwa kuhitimu kwako Amo. Wewe ni nyota katika utengenezaji,” Nyamu aliandika.

 Katika picha hizo, Nyamu alionekana amefurahia ukaribu wake na baba wa wanawe – Samidoh huku wamekumbatiana kwa mahaba yasiyojua kupoa wala kufa.

Wanafamilia wa Samidoh pia walionekana kufurahia uwepo wa Nyamu miongoni mwao, na kuwaacha watumizi wa mitandao ya kijamii wakizungumza, wengine wakisema kuwa Nyamu hatimaye amefanikiwa kupata nyota ya mashemeji zake, huku Edday akizidi kuonekana kusahaulika asteaste.

“Hapa ndio unaonaga Kama Mungu hayupo coz nothing but prayers,” Eukenees aliandika, akitumia kauli ambayo Edday anapenda kuitumia sana kwenye machapisho yake.

“Hata kama ni wewe familia ya Samidoh utachagua pesa ama maombi?” Deetonie aliandika akionekana kurejelea kwenye kauli ya Edday na ukwasi wa Nyamu.

“Chochote Sam anawaza kuhusu familia yake ya kwanza hasa watoto sijui,,” Diana Dee Kui aliuliza.

😂😂😂😂Bado wa ooh he will never leave his wife for you mko😂😂😂Mwanamke kama hataki kukupenda oa tena buana😂😂😂life is short to be unhappy,” Wakhungu Monica alisema.

“#nothingbutprayers hii ilienda kabisaa na hairudi😂😂😂😂😂” Sheekow Maina alisema akirejelea kauli ya Edday.

Nyamu alionekana na familia ya Samidoh ikiwa ni siku chache tu baada ya kuonekana akiwa amevimba usoni ambapo baadhi ya mashabiki walikisia kwamba huenda aliadhibiwa na Samidoh licha ya Nyamu mwenyewe kukanisha madai hayo.