Ujumbe wa Edday Nderitu uliowaacha wanamitandao na hisia chungu nzima

Anajulikana pia kwa kumsaidia na kumuunga mkono Samidoh katika taaluma yake ya muziki.

Muhtasari
  • Aliwaambia kwamba baada ya kila mtu kunusurika, wanapaswa kujifundisha jinsi ya kustawi.
  • Alisema hii ni kwa sababu kila mtu anastahili kuwa na furaha baada ya kupitia kila kitu kilichojaribu kuwaangamiza.
Bi Edday Nderitu
Image: FACEBOOK

Edday Nderitu anajulikana zaidi kama mke wa mwanamuziki wa nyimbo za Kikuyu Samidoh Muchoki na mama wa watoto watatu.

Anajulikana pia kwa kumsaidia na kumuunga mkono Samidoh katika taaluma yake ya muziki.

Kwa muda sasa hajaelewana na mumewe Samidoh tangu Samidoh alipokutana na Karen Nyamu ambaye wamezaa naye watoto wawili.

Kwa sasa Eddy yuko Marekani ambako aliapa kwamba huenda hatarejea Kenya hivi karibuni.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa facebook alichapisha ujumbe akiwapa Wakenya ushauri ambao umewaacha wengi kukubaliana naye.

Aliwaambia kwamba baada ya kila mtu kunusurika, wanapaswa kujifundisha jinsi ya kustawi.

Alisema hii ni kwa sababu kila mtu anastahili kuwa na furaha baada ya kupitia kila kitu kilichojaribu kuwaangamiza.

Wakenya walikuwa kwenye sehemu ya maoni wakisema wanakubaliana naye kwani wengine walimtakia nguvu zaidi na kila kitu kitakuwa sawa hivi karibuni.

"Baada ya kuokoka, jifundishe jinsi ya kustawi. Kwa sababu unastahili kuwa na furaha baada ya kupitia kila kitu ambacho kilijaribu kukuangamiza ..."

Bi Edday nderitu,alichangia katika mjadala ulioendelea mitandaoni kuhusu madai tata kwamba mwimbaji huyo wa Mugithi alimshambulia mpenzi wake mwingine na mzazi mwenzake, Karen Nyamu.

Wikendi, picha ya seneta Karen Nyamu akiwa na uso wenye michubuko ilisambaa kwenye mitandao ya kijamii na kuzua uvumi kwamba alikuwa mwathiriwa wa dhuluma za nyumbani. Baadhi ya wanamitandao hata walidai kuwa seneta huyo alipigwa na mpenzi wake Samidoh, madai ambayo tayari ameyapuuzilia mbali.