AKOTHEE THE GOAT

Jina langu lina maana ya ufanisi - Akothee

“Mimi ndiye “The Goat”, wananiiga kama mwelekezi wao,” Akothee aliposti

Muhtasari

•Wakuza maudhui mashuhuri, wanatafuta umaarufu, wafuasi  na umuhimu kwa sababu wangeeleza maisha yao wenyewe kwa majina yao hakuna  wa kuwapa umakini.

Akothee katika picha akicheza mprira wa kandanda
Akothee katika picha akicheza mprira wa kandanda
Image: Akothee // INSTAGRAM

Mwanamuziki Esther Akoth maarufu Akothee ameeleza kuwa jina lake linamaanisha mafanikio.

Katika mtandao wake wa Instagram, mama huyo wa watoto watano ameeleza kuwa ukisikia mtu akitaja jina Akothee au akijaribu kumuiga, basi ujue kwamba yeye ni mwelekezi wao.

Wakati utasikia yeyote akitaja Akothee au wakijiiga naye, jua tu mimi ndiye mwelekezi wao wa kuigwa, maana kamili ya ufanisi,” Aliposti.

Aliendelea  kueleza kuwa baadhi ya watu wanajua mambo yake ila mwenyewe hawajui huku akieleza mshindani wake mkubwa ni yale aliyofeli.“ Wanajua mambo yangu ila mimi mwenyewe hata siwajui wao. Mshindani wangu mkubwa ni kufeli kwangu, huwa nahakikisha kuwa nimerekebisha chochote ambacho huenda nimepoteza.”

Akothee aliendelea na kusema kuwa ukisikia watu wakimtaja unaweza kusaili “GOAT”, ambapo aliendelea kuwa jina Akothee peke yake linatosha kukupatia umaarufu kwa dakika mbili.

Mwimbaji huyo aliyenaswa kwenye picha akidensi shambani na akicheza mpira alisema kuwa Akothee ndiye motisha wako, ila akakaidi kuwashukuru wenye wivu. “ Akothee ni hifadhi ya makumbusho yanayosonga, mtu mashuhuri pekee ambaye hawezi kununua bidhaa katika duka kuu, au kushuka katikati mwa jiji.”

Mama huyo mwenye umri wa miaka 43 waliwashutumu baadhi ya wakuza maudhui, ambapo alisema kuwa, wengine wanafuata umashuhuri na wafuasi kwa kuyakuza maudhi yao, akisema kuwa wangefanya hivyo kwa kutumia jina lao kamili hakuna mtu angewapa umakini.

“ Wakuza maudhui mashuhuri, wanatafuta umaarufu, wafuasi  na umuhimu kwa sababu wangeeleza maisha yao wenyewe kwa majina yao hakuna  wa kuwapa umakini, aliendelea.

Akothe aliendelea na kujipongeza ambapo alisema hukwa huwa anasambaa kila wakati katika mitandao kwa kuwa kuwa kwenye sherehe kila mahali.