Alikiba ana 60% kwenye maisha yangu - Niffer, mrembo anayetajwa kuwa mpenzi mpya

“Alikiba ana part kubwa sana kwangu. Ali ana asilimia labda 60. Ni mtu mzuri kwangu, yaani ni mtu wa kipekee,” Niffer alisema.

Muhtasari

• Hata hivyo, Niffer alisema kuwa yeye si chanzo cha kuzuka mporomoko kwenye penzi la Kiba na mkewe Amina Khelef.

• Niffer alisema kuwa anajua yeye ni mtu mzuri na hawezi kumsababishia mwanamke mwenziwe uchungu.

Niffer afunguka uhusiano wake na Alikiba
Niffer afunguka uhusiano wake na Alikiba
Image: Instagram

Niffer, mrembo ambaye ni mjasiriamali wa duka la nguo nchini Tanzania na ambaye katika siku za hivi karibuni amekuwa akitajwa sana kuwa chanzo cha ndoa ya Alikiba na mkewe kutoka Kenya Amina Khelef kuyumba amefunguka uhusiano wake na msanii huyo.

Katika mahojiano ya kipekee na Ayo TV, Niffer amekanusha vikali kwamba hajahusika kwa njia yoyote kuwa chachu mbaya kwenye uhusiano uliogonga mwamba wa msanii huyo wa  Bongo Flava, huku akisema kuwa hata hamfahamu Amina.

Alipoulizwa kama yeye mwenyewe amewahi hisi kana kwamba Amina ana chuki naye, Niffer alisema kuwa hajawahi hisi hivyo kwa sababu hata hawajuani na mwenyewe kutoka ndani ya moyo wake anafahamu kwamba ni mtu mzuri, wala asignependa kumfanyia Amina ukatili wa kumchukulia mume wake.

Hata hivyo, Niffer alimsifia Alikiba pakubwa, akisema kuwa mpaka kufikia hatua aliyoifikia kimaisha sasa hivi, mchango wa Alikiba kwa maisha yake umekuwa kama wa asilimia Zaidi ya 50.

“Alikiba ana part kubwa sana kwangu. Watu wengi wanaona kwamba ukiongea kitu wanakichukulia negative sana, lakini kuna ule msemo unasema mtu mpe maua yake. Mtu akiwa mzuri kwako kwa nini ukae kimya tu kisa unaogopa watu watasema?” aliuliza.

“Ali amechangia part kubwa sana kwenye maisha yangu. Na kusema ukweli naweza nikasema hata huyu Niffer ambaye niko sasa hivi, Ali ana asilimia labda 60. Ni mtu ambaye hawezi kubali eti umeposti kapicha kako ka aibu halafu akuambie haya ‘nice picture’. Hapana, atakwambia wewe ni Muislam, hutakiwi kufanya hivi,” Niffer alimpa maua yake Alikiba.

Niffer kando na biashara pia amemtaja Alikiba kuwa mwalimu wake mzuri ambaye amekuwa akimfunza jinsi ya kuzungumza haswa kwenye mahojiano.

“Ni mtu ambaye hata nikifanya interview yangu kule nimeboronga ataniambia, ‘hapana, usiseme hivi wakati mwingine. Jaribu kuwa na faragha Zaidi’. Ni mtu mzuri kwangu, yaani ni mtu wa kipekee,” Niffer alisema.