Pengo la Rayvanny WCB Wasafi kuzibwa Januari 2024 - Diamond atangaza

Baada ya Rayvanny kuondoka Wasafi, Diamond amesalia na wasanii watatu tu – Zuchu, Mbosso na Lavalava huku wawili tu wakiwa ndio pekee wanaofanya vizuri.

Muhtasari

• Pia alisema kuwa atakaowapa nafasi ni wasanii wengine wa Wasafi pamoja na wasanii wa nje ambao anawaheshimu.

Diamond kuongeza msanii mpya Wasafi Januari mwaka kesho.
Diamond kuongeza msanii mpya Wasafi Januari mwaka kesho.
Image: Screengrab//YouTube

Afisa mkuu mtendaji wa kampuni ya WCB Wasafi Diamond Platnumz ametangaza kwamba Januari mwaka kesho atamzindua msanii wake mpya katika lebo hiyo kuchukua nafasi ya Rayvanny ambaye aliondoka mwaka jana na kuanzisha lebo yake ya Next Level Music.

Kupitia aya ndefu alizochapisha kwenye instastories zake, Diamond alisema kuwa anaanza Julai hii kuachia miziki yake ikiwemo ni collabo za nje na ndani ya Afrika na kuwaahidi mashabiki wake kuwa atashikilia nafasi ya kwanza kwenye chati za muziki kwa miezi hiyo yote hadi mwisho wa mwaka.

Kisha Januari mwaka jesho, atachukua pumziko kidogo na kumzindia msanii wake mpya ambaye ataendeleza kutoka hapo na kuipeperusha bendera ya WCB Wasafi.

“Januari 2024 nitampisha msanii wangu mpya,” Diamond alisema.

Pia alisema kuwa atakaowapa nafasi ni wasanii wengine wa Wasafi pamoja na wasanii wa nje ambao anawaheshimu.

Msanii huyo alionekana kuachia pembe zote nje tayari kwa vita akiwasuta baadhi ya washikadau kwa kumkejeli kuwa ameishiwa na ubunifu wa nyimbo nzuri.

INSTAGRAM
Image: MOSES SAGWE

Hata hivyo, Diamond aliwapiga makombo vikali akisema kuwa anarudi kwa kishindo cha aina yake kuenda Zaidi katika rubaa za kimataifa, lakini pia hakufutilia mbali uwezekano wa kuwashirikisha wasanii wa Bongo haswa kipindi hiki ambapo anaeleka kuzindua tamasha la Wasafi.

“Haimanishi eti ndio kupuuza kanisa kufanya ngoma na rafiki zangu tokea Tanzania ama East Africa. Nazo zina umuhimu kwa waswahili wenzangu haswa msimu kama huu wa Wasafi Festival unavyokuja. Hivyo tegemeeni pia kumwagika kwa nyingi tu za kutosha,” Diamond alisema.

Baada ya Rayvanny kuondoka Wasafi, Diamond amesalia na wasanii watatu tu – Zuchu, Mbosso na Lavalava huku wawili tu wakiwa ndio pekee wanaofanya vizuri na kuiendeleza legacy ya lebo hiyo inayotajwa kuwa kubwa Zaidi katika ukanda huu.