KIATU KIREFU KIPO

Viatu vya kumpwerepweta Eric Omondi katika ziara ya Tz viazua vichekesho

Hakuna wa kutoshea ndani ya viatu vyangu - Eric Omondi

Muhtasari

• Saa chache zilizopita, Eric Omondi aliposti kuwa safari imekuwa ndefu ila alifanikiwa kufika Dar es Salaam salama, ambapo alidakia kuwa siku itakayofuata ataelekea katika mji wa Dodoma.

Image: Eric Omondi// INSTAGRAM

Katika kanda ya video inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii, mkuza maudhui Eric Omondi alitua katika uwanja wa ndege nchini Tanzania huku akiwa amevalia viatu virefu kuliko nyayo zake.

Awali, mchekeshaji huyo alitoa video nyingine akiwaeleza wakaazi wa mji wa Dodoma nchini Tanzania kuwa wajiendae maana pia naye alikuwa akijiandaa kusafiri huko siku ambayo ingefuata.

TANZANIA !!! DODOMAAA!! Nipo Njiani. Tuonane Kesho!! Hakuna anayeweza kutoshea ndani ya viatu vyangu kamwe,” Msanii huyo aliposti katika mitandao yake ya kijamii saa chache kabla ya kuabiri ndege kueleka Tanzania.

Video hiyo iliibua masuala ibuka kwa wanamitandao, ambapo pia majibu na mijadala yaliibuka kutokana nayo. Mtangazaji wa redio, Mulamwah alimtania kwa kumwuuliza kuwa alikuwa ameenda kuona “ Titanic”.

Katika maoni kwa mwanamitandao mwingine alitoa maelezo yake ya kitani kuwa viatu kama hivyo ni vya kusafirisha mihadarati, huku naye mwingine pia akisaili kuwa viatu kama hivyo vinapaswa kulipiwa tikiti, aliposema kuwa angepaswa kulipia tikiti mbili za kuabiri ndege.

Saa chache zilizopita, Eric Omondi aliposti kuwa safari imekuwa ndefu ila alifanikiwa kufika Dar es Salaam salama, ambapo alidakia kuwa siku itakayofuata ataelekea katika mji wa Dodoma. “ Safari imekuwa ndefu, ila tunefika Dar Salama...Dodoma kesho,” aliendeleza.

Sababu ya kuvaa viatu hivyo bado haijaweza kubainika, ambapo tunatarajia maelezo kutoka kwake atakaporejea nchini.