Wimbo mpya wa Bahati 'Diana' wapata views milioni 1 YouTube ndani ya saa 48

Wimbo huo wa Bahati na Bruce Melodie ulikuwa umeondolewa YouTube kutokana na mzozo wa maudhui.

Muhtasari

• Wimbo huo ulipoachiwa mara ya kwanza, ulipokelewa kwa kishindo na mashabiki, lakini muda mfupi baadaye, ulitoweka kwenye chaneli ya YouTube ya Bahati.

• Saa chache tu baadaye,mwimbaji huyo alitangaza kurejeshwa rasmi kwa "Diana" kwenye chaneli yake ya YouTube, ambapo sasa inaweza kutazamwa na wafuasi wake.

Mwanamuziki wa Rwanda Bruce Melodie na Bahti kutoka Kenya.
Mwanamuziki wa Rwanda Bruce Melodie na Bahti kutoka Kenya.
Image: INSTAGRAM/ BAHATI

Wimbo wa hivi punde wa mwanamuziki, Bahati 'Diana' umeweza kufikisha zaidi ya views milioni 1 chini ya saa 48 na kuimarisha umaarufu wake, kuthibitisha tena nafasi ya Bahati kama mmoja wa msanii anayeongoza katika muziki ya Kenya.

Wimbo huo ulikuwa umeondoloewa YouTube kutokana na mzozo wa maudhui. Hata hivyo, wimbo huo umerejea kwa kishindo na kuibua msisimko miongoni mwa mashabiki wa mwanamuziki huyo.

Ushirikiano kati ya Bahati na supastaa wa Rwanda Bruce Melodie kwenye wimbo wa "Diana" ulionekana kuwa muelewano kati ya wasanii hawa, na kuwavutia wasikilizaji kwa uwiano wake wa kipekee wa aina za muziki.

Wimbo huo ulipoachiwa mara ya kwanza, ulipokelewa kwa kishindo na mashabiki, lakini muda mfupi baadaye, ulitoweka kwenye chaneli ya YouTube ya Bahati.

Akielezea kufadhaika na kutamaushwa kwake kwenye akaunti yake ya  Instagram, Bahati alionekana kuishutumu kampuni moja ya usambazaji wa muziki nchini kwa kudukua akaunti yake na kufuta "Diana."

Alitaja kampuni hiyo kama walaghai na kuitaka serikali ya Kenya kuingilia kati, akisisitiza haja ya hatua za udhibiti kulinda waundaji wa maudhui.

Bahati, katika ujumbe kwenye Instagram yake, alitoa shukrani zake kwa mashabiki na akafichua kuwa mzozo kati yake na kampuni hiyo ulikuwa umesuluhishwa kwa njia ya amani.

Mwimbaji huyo alitangaza kurejeshwa rasmi kwa "Diana" kwenye chaneli yake ya YouTube, ambapo sasa inaweza kutazamwa na wafuasi wake.

Akikubali kuwepo kwa uhusiano wa awali wa ushirikiano na kampuni hiyo, Bahati alielezea nia yake ya kufanya kazi pamoja nao ili kuendelea kuchangia ukuaji wa tasnia ya muziki barani Afrika.

Huku wimbo huo ukiendelea kupanda chati za Trending kule Youtube, "Diana" sasa ameshika nafasi ya 7 katika kitengo kinachovuma nchini Kenya.