Pritty Vishy atishia kuanika picha na video chafu za mtangazaji maarufu nchini

“Unajua wewe, nitakuanika wewe. Unaona huto tuvideo zako ukijiingiza nini.. kuwa makini sana na mimi. Nina chai na nitaipakua" - Vishy alitishia.

Muhtasari

• Vishy alisema kuwa endapo Atieno hatokoma kumdhihaki mitandaoni, atamuanika kwa kuchapisha picha na vide zake za utupu

Pritty Vishy atishia kuchapisha video chafu.
Pritty Vishy atishia kuchapisha video chafu.
Image: Instagram

Pritty Vishy ametishia kuchapisha picha na video za mtangazaji maarufu wa redio humu nchini endapo ataendeela kumchokonoa.

Katika mazungmzo na mwanablogu Mungai Eve, Pritty Vishy alisema kuwa amekuwa akijaribu kujizuia sana dhidi ya mashambulizi ya mtangazaji huyo wa kike mitandaoni lakini sasa ni kama yako karibu kumfika kwenye koo na hatoendelea kumeza Zaidi bali atalazimika kutema.

Alisema kuwa wamekuwa wakitofautiana na mtangazaji Atieno mitandaoni tangu mwaka jana na mtangazaji huyo wa zamani wa kitu kimoja cha redio humu nchini ameenda sana mpaka kumshambulia kuhusu muonekano na maumbile ya mwili wake.

Vishy alisema kuwa endapo Atieno hatokoma kumdhihaki mitandaoni, atamuanika kwa kuchapisha picha na vide zake za utupu

“Unajua wewe, nitakuanika wewe. Unaona huto tuvideo zako ukijiingiza nini.. kuwa makini sana na mimi. Nina chai na nitaipakua. Siku moja nitaamka tu hivi akili iniambie Pritty post hiyo video chafu na nitaichapisha… na video hiyo ni nzuri…” Vishy alisema kwa vitisho.

Mwanablogu huyo alisema kuwa amekuwa akinyamazia masimango ya Atieno dhidi yake lakini yamekuwa Zaidi sasa baada ya mtangazaji huyo kuzidi mipaka na kuanza kukejeli jinsi anavyoonekana kweney baadhi ya mavazi yake.

“Atieno, kuwa makini sana, acha kabisa kuzurura kwenye biashara zangu. Mimi huwa siko katika baishara zako na sijawahi na siwezi.”