Diamond adhibitisha Zuchu kuwa na mimba yake? Adai mchumba wake kujifungua Januari

Diamond na Zuchu kwa muda mrefu wamekuwa wakionesha dalili zote za kuchumbiana na miezi michache nyuma Zuchu alisemekana kuwa mjamzito.

Muhtasari

• Msanii huyo aliwashukuru mashabiki wake kwa kuifanya ngoma yake mpya ya ‘My Baby’ kushikilia nafasi ya kwanza kwenye YouTube ikiwa ni siku mbili tu baada ya kuiachia.

Mama Dangote akanusha Diamond kutoka kimapenzi na Zuchu.
Mama Dangote akanusha Diamond kutoka kimapenzi na Zuchu.
Image: Screengrab//YouTube

Msanii Diamond Platnumz amewaacha wafuasi wake kwenye mtandao wa Instagram kwenye njia panda baada ya kudai kwamba mchumba wake ni mjamzito.

Msanii huyo kupitia Insta story yake, aliandika kwamba mchumba huyo wake ambaye hata hivyo hakumtaja kwa jina, anatarajia kujifungua mwezi Janauri mwakani.

Diamond aliandika ujumbe kama wa kuwaambia kwaheri mashabiki wake akisema kuwa ni mpaka Janauri mwakani wakati atatarajia kuitwa baba kwa mara nyingine tena.

“Haya tukutane Januari mwakani mchumba anapoenda kujifungua,” Diamond aliandika.

Msanii huyo aliwashukuru mashabiki wake kwa kuifanya ngoma yake mpya ya ‘My Baby’ kushikilia nafasi ya kwanza kwenye YouTube ikiwa ni siku mbili tu baada ya kuiachia.

Msanii huyo wiki jana alitoka vitisho vikali kwa washindani wake wa muziki akisema kuwa atarudi kwa kishindo na kukaa kwenye namba moja kwenye chati za muziki kuanzia Julai hadi Januari mwakani.

Baada ya kidokezo hicho, baadhi walihisi moja kwa moja mchumba mjamzito atakuwa Zuchu, msanii wake ambaye amekuwa akihusishwa kutoka kimapenzi naye kwa muda mrefu.

Ikumbukwe miezi michache nyuma, watu kadhaa akiwemo Juma Lokole walisema kwamba Zuchu ni mjamzito kwa Diamond lakini msanii huyo hajaonekana kudhibitisha wala kukanusha hilo.

Kuanzia mapema mwaka jana, Diamond na Zuchu wamekuwa wakionesha dalili zote kuwa ni wapenzi, ikiwemo mpaka katika hafla ya uzinduzi wa albamu ya Juma Jux ambapo Diamond jukwaani aliimba kionjo cha ngoma ambayo Zuchu alimshirikisha Jux na kumtaja kuwa ‘mke wangu’ – tamko ambalo liliwakera wengi Waislamu wakiongozwa na Mwijaku aliyemtaka Diamond kutubu kwa kumuita mwanamke ‘mke wangu’ licha ya kwamba hawajafunga nikkah rasmi kwa mujibu wa tamaduni za dini hiyo.